Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

KANDA YA KATI (DODOMA) YAVUKA MALENGO MAKUSANYO YA KODI YA PANGO LA ARDHI

kat1
Kamishna wa Ardhi msaidizi – Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na  Waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi yake, Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki. Kushoto kwake ni Mwanasheria na Afisa Ardhi mwandamizi; Jane Kapongo na kulia kwake ni Msajili wa Hati katika kanda hiyo; Geoffrey Mauya.

kat2
Vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu  Kodi ya Pango la Ardhi vikigaiwa kwa Wananchi katika Stand ya Mabasi mjini Dodoma
kat3
Kamishna wa Ardhi msaidizi – Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na  A Fm Radio –  92.9 – Dodoma;  kuhusu Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki.
kat4
Kamishna wa Ardhi msaidizi – Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na  Maisha Radio –  100.1 – Dodoma;  kuhusu Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki.
………………………………………………
Kanda ya kati (Dodoma) yakusanya kiasi cha Tshs. 1,426,273,033.70 ya Makusanyo ya Kodi ya Pango la Ardhi, sawa na 204% ya malengo na hivyo kuvuka malengo iliyopangiwa. Kamishna Msaidizi wa Ardhi, kanda ya kati Dodoma; Hezekiel Kitillya ameeleza wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.  
Kamishna Kitillya alisema; tathimini iliyofanyika ni ya mpaka 31 Mei, 2017. Malengo ya Makusanyo yaliyokuwa yamepangwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 – 30 Juni, 2017 yalikuwa ni kukusanya kodi ya Tshs. Bilioni 111.77, ambapo kati ya kanda nane za ardhi zilizopo nchini, kanda ya kati ilipangiwa kukusanyaTshs. Milioni 700.
Vile vile,  baadhi ya Halmashauri tayari zimeshavuka malengo ya makusanyo zilizowekewa, kama vile Manispaa ya Dodoma,  malengo yalikuwa Tshs. 200,000,000/= na makusanyo yakawa;  Tshs.678,804,841.40, Manispaa ya Singida, malengo yalikuwa Tshs. 200,000,000/= na makusanyo yakawa Tshs.308,392,069.17 na Halmashauri ya Manyoni, malengo yalikuwaTshs. 100,000,000/= na makusanyo yakawa Tshs. 117,200,000.00. Pia Halmashauri nyingine za Wilaya ya Itigi, Chamwino, Bahi; nazo zimeshavuka malengo na nyingine zilizobaki zikikaribia kufikia malengo.
Akieleza moja ya mkakati muhimu ambao umewezesha kanda yake kuvuka malengo ni pamoja na kusambaza hati za madai Demand notes. Alisema; “Halmashauri zote zilielekezwa kuandaa na kusambaza hati za madai kwa wadaiwa wakubwa sugu”.
Akizungumzia moja ya changamoto Kuu inayokabili zoezi la Makusanyo; Alisema ni Wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu tofauti ya Kodi ya Pango la Ardhi na Kodi ya Majengo, ambapo Wananchi wengi hudhani wakishajenga nyumba na kuanza kulipa kodi ya jengo, hawapaswi tena kulipa kodi ya pango la Ardhi.
Aidha, Kamishna Kitillya ametoa wito kwa Wananchi kuhamasika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa mujibu wa Sheria na kwa Maendeleo ya Taifa.  Aliongeza kuwa; “Sasa Kodi ya Pango la Ardhi imeboreshwa kwa kumuwezesha mwananchi kutambua kiasi anachodaiwa na kufanya malipo hayo kieletroniki, kwa kutumia Tovuti ya Wizara au simu kwa tigo pesa au m-pesa, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Mwananchi alilazimika kufika katika vituo vya malipo, katika Halmashauri yake”.
Kanda yakati (Dodoma) inahudumia mikoa miwili (2) Dodoma na Singida yenye jumla ya Halmashauri kuminatano (15).
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget