Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MASAU BWIRE:TUMEJIANDAA KUIFUNDISHA SOKA SINGIDA UNITED UWANJA WA MABATINI JIONI YA LEO


maxresdefault-1

Timu ya Ruvu shooting ya Mkoani Pwani inayojulikana kama Leicester City jioni ya Leo itashuka  kucheza mchezo wa kirafiki na Matajiri wa Singida United mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Mabatini Mlandizi majira ya saa kumi  1:00 jioni.

Akizungumza na Mtandao wa mapema asubuhi Leo msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire,amesema kuwa wamejipanga vizuri na kitakuwa kipimo tosha kwao kuelekea msimu wa Ligi wa 2017-18 na wanaimani kuwa wataibuka na ushindi mnono.

“Leo tunataka kuweka historia ya kushinda magoli mengi kwani tuna mabomu ya Nyuklia kama yale ya Korea Kaskazini yanayoitisha dunia kwa sasa na sisi tuna full mziki kwani tuna wachezaji wazuri tuliowasajili pamoja na hao wa zamani hivyo Singida United watatafuta njia ya kutokea na tutawakaribisha kwa kipigo kabla ya ligi kuanza’amesema Bwire
Hata hivyo Msemaji huyu amesema kuwa Mchezo utakuwa mzuri kwani Singinda wanafundishwa na kocha bora pamoja na kufanya usajili mzuri wa wachezaji wazoefu na michuano mbalimbali hivyo wataleta upinzani kwao ila haiwezi kuwazuia kushindwa kupata ushindi kwao.

Kwa upande wa Nahodha wa klabu ya Singida United,Nizar Khalfani amesema kuwa mchezo huo wanaujukulia kwa umakini zaidi na wanajua wanakutana na timu ya aina gani huku wakiwa na kumbukumbu ya Kupoteza mchezo wao dhidi ya Lipuli FC ya mkoani Iringa.

“Tumejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kwa maelekezo ya kocha Mkuu Hans Van Der Pluijm,kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani kocha anaendelea kutafuta kikosi cha kwanza ikizingatiwa wachezaji wengi ni wapya”Amesema Khalfani
Singida United imepanda msimu huu na tayari imeanza kuonesha cheche kwa kufanya usajili mkubwa kwa kuwanyakuwa wachezaji bora wenye uzoefu na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara pamoja na ukanda wa bara la Afrika kwani ina kocha bora mwenye Rekodi Tanzania na Afrika akiwa na Yanga aliweza kutetea taji la Ligi Kuu mara mbili na kuchukua kombe la FA na Ngao ya Hisani na akiwa nchini Ghana aliipa mafanikio timu ya Berkmu Chelsea ambayo ilifika katika hatua ya Ligi ya Mabingwa.

Singida United huu utakuwa mchezo wa nne wa Kirafiki kucheza wakiwa wameshacheza na Pamba ya Mwanza na kushinda magoli 5-0,Alliance School wakashinda 2-0 na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Lipuli FC 1-0 na wanatarjia kucheza mechi moja siku ya Jumamosi Agosti 5 dhidi ya Mabingwa wa Kihistoria Yanga na watasafiri kwenda nje ya nchi kucheza michezo mbalimbali ya kujipima nguvu zaidi kabla ya kuanza kipute cha Vodacom Ligi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget