Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

UHAMIAJI WAMALIZA UTATA WA URAIA WA KARIA

Michuzi Karia
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda akiongea na Vyombo vya Habari kuhusu matokeo ya uchunguzi wa suala la utata wa uraia wa Ndugu Wallace John Karia, ambaye ni mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF. Kutokana na pingamizi lililowekwa na Wakili Imani Madega, mgombea mwingine wa nafasi hiyo.
…………………………..
Idara ya Uhamiaji Tanzania, imemaliza utata juu ya uraia wa mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, baada ya kusema ni raia halali wa Tanzania tofauti na wengine wanavyosema.
Uhamiaji wamefikia hatua hiyo baada ya Karia kuwekewa pingamizi na mgombea mwenzake, Imani Madega ambaye alisema mgombea huyo si Mtanzania, bali ni Msomalia, hivyo hana vigezo vya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Msemaji Mkuu wa Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, amesema: “Baada ya kupokea taarifa hiyo, tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba Karia ni Mtanzania na wala si Msomalia.
“Karia alizaliwa hapa nchini ambapo mama yake ni Mtanzania wakati baba yake ni Msomalia. Kutokana na msingi huo, Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo la 2002 na kanuni zake. 
“Wakati huohuo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi. Ni hitaji la kisheria chini ya kifungu cha 7(1), pale mtu anapokuwa  na uraia wa nchi mbili kuukana uraia wa nchi moja anapofikisha umri wa miaka 18 hatua ambayo Karia aliitekeleza na kuthibitishwa ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.”
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget