Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MGODI WA GGM KUBURUZWA MAHAKAMANI KUTOKANA NA MADAI YA KUTOKULIPA DOLA ZA KIMAREKANI ZAIDI YA MILIONI 11.04 KWENYE HALMASHAURI MBILI MKOANI GEITA


Baadhi ya madiwani wa Baraza hilo,wakifuatilia taarifa ya mwanasheria wa halmashauri juu ya madai ambayo wanahudai mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)
Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo,Leornad Kiganga
Bugomola,akielezea msimamo wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo juu ya madai ya mgodi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akijibu baadhi ya maswali.
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini.Constatine Kanyasu akichangia ajenda ya swala la malipo ya mgodi kwa halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa mgodi wa GGM Kwenye baraza Hilo
Bw Joseph Mangilima akitoa ufafanuzi juu ya madai ambayo yanadaiwa na Halmashauri.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE



Halmashauri ya mji wa Geita imeitaka kampuni ya madini ya dhahabu ya Geita (GGM) kulipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni 11.045  ambazo ni madai ukwepaji wa kodi ya huduma kwa kipindi cha mwaka 2004 hadi 2013 nakuipa muda wa mwezi mmoja endapo itashindwa itaupeleka Mgodi Mahakamani.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Eng. Modest Apolinary,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola.
Mgodi wa GGM ulianza uzalishaji mwaka 2000 na kuingia makubaliano na Wizara ya nishati na madini ya kulipa dola 200,000 kwa halmashauri kila mwaka lakini inadaiwa haikulipa hadi mwaka 2004 kwa madai kuwa halmashauri haina sheria inayoelekeza walipwe kiasi hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amesema kuwa wametoa siku 30 fedha zilipwe na endapo hawatalipwa basi wataupeleka mgodi Mahakamani kwakuwa sheria zipo wazi inayowataka kulipa asilimia 0.03
Awali akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwanasheria wa Halmashauri ya mji Queen Luvanda amesema Madai hayo yanatokana na kodi ya huduma ambayo kampuni ilipaswa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka 2004 Halmashauri ilitunga Sheria ndogo ya kodi ya huduma ya asilimia 0.03  ya mauzo ya mwaka  na kuanzia sheria itungwe mgodi hawakulipa asilimia 0.03 bali walilipa dola laki mbili kuanzia mwaka 2004 hadi 2013 kinyume na maelekezo ya sheria inavyosema.
Maneja Kitengo cha Mahusiano katika Mgodi wa GGM Joseph Mangilima amesema sheria ya kodi ya huduma ilitungwa mwaka 2004 na ikaanza kufanya kazi mwaka 2005 na Kampuni ilikua ikilipa dola 200,000 kila mwaka kwa mujibu wa sheria

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget