Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

YANGA KUZIDI KUTESTI MITAMBO YAKE DHIDI YA RUVU SHOOTING JUMAMOSI HII



Kikosi cha timu ya Yanga kinataraji kushuka dimbani siku ya jumamosi kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani.

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa kwenye maandalizi ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Mbali na mchezo huo utakaopigwa siku ya jumamosi pia kikosi cha Yanga kinatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki na timu ya Mlandege FC ya Zanzibar,mechi itakayochezwa siku ya jumapili ya tarehe 13 ya mwezi huu kwenye uwanja wa  Amani huko Zanzibar.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget