Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MWENYEKITI WA BODI YA NHIF MHE. MAKINDA ATEMBELEA BANDA LA NHIF KATIKA MAONESHO YA NANENANE DODOMA NA KUSISITIZA UMUHIMU WA KILA MWANANCHI KUWA NA BIMA YA AFYA.

Mwagala
1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mhe. Anne Makinda akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la NHIF jijini Dodoma alipotembelea maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni jijini humo.
2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga na viongozi wengine wa NHIF wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF alipotembelea banda hilo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane.
3
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda
akisalimiana na mmoja wa maofisa wa NHIF waliokua wakishiriki maonesho
ya Nanenane Jijini Dodoma.
4
Meneja wa NHIF mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea jambo
kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda ambaye
pia alitembelea banda hilo kama mgeni Rasmi wa maonesho hayo ya
Nanenane yaliyokua yakifanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya
Nzuguni.
……………………………
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mhe. Anne Makinda ametembelea Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo. Mhe. Makinda alisisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila siku na kuepukana na umaskini.
Alisema ‘…. tunajua kuwa katika zama hizi tunatakiwa kuchapa kazi kama Mhe. Rais wetu anavyotuhimiza, lakini ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi anapougua”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga amesema NHIF imejipanga kutoka na kwenda kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo. Alisema kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO AFYA KADI. “Mfuko umeanza kufanya usajili kwa wingi katika maeneo mbalimbali karibu na watu walipo ambapo kila mtoto anachangiwa sh. 50,400 tu kwa mwaka” alisema Bw. Konga.
Huduma hii ya TOTO AFYA KADI imezinduliwa  rasmi na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wiki iliyopita ambaye alisema kuwa watoto ambao ni asilimia 51 ya watanzania wote wanahitaji kuwa na uhakika wa matibabu na alihimiza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma hiyo.
Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma, Bi. Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonesho hayo. Ameongeza kusema kuwa umma uko tayari na wamejipanga kuendeleza kampeni hiyo katika maeneo ya karibu zaidi na wananchi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget