KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki
na Kati, Azam FC, imeshinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa
maandalizi ya msimu ujao, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho wa
kikosi hicho kabla ya kuelekea nchini Uganda kuweka kambi ya siku 10
katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL),
Bao pekee la Azam FC limefungwa na
beki kisiki na Nahodha Msaidizi, Aggrey Morris, dakika ya 57 kwa njia
ya mkwaju wa penalti kufuatia mshambuliaji Wazir Junior kuangushwa
kwenye eneo la hatari.
Azam FC iliutawala mchezo huo kwa
kiasi kikubwa hasa kipindi cha pili ikicheza soka safi la pasi na kasi
huku ikishuhudiwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Junior, Enock
Atta, Yahya Zayd, Bruce Kangwa, waking’ara vilivyo kwa kupeleka
mashambulizi makali langoni mwa KMC.
Mara baada ya mchezo huo, kikosi
cha Azam FC kinatarajia kupumzika kwa siku moja kabla ya keshokutwa
alfajiri kuanza safari ya kuelekea nchini Uganda itakapocheza mechi nne
za kirafiki dhidi ya KCCA, Vipers, URA na SC Villa, zote zikiwa timu
kongwe za nchini humo.
Post a Comment