Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw.
James Ihunyo (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa pamoja na
wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula,iliyopo katika kijiji cha
Mkula wilaya ya Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw.
James Ihunyo (aliyesimama) akihimiza jambo wakati akizungumzia kukamatwa
kwa wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea
kusimamia mkopo wa TADB.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji, Bw. Adam Kamanda (kushoto) akiongea kwa uchungu kitendo cha
wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea
kusimamia mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 790 zilizotolewa TADB.
Baadhi ya wanachama na wanakijiji
wa kijiji cha Mkula wakifuatilia mazungumzo wakati wa kikao cha pamoja
kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo, wawakilishi wa Benki ya Kilimo na wanachama
wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji
cha Mkula wakitoa maoni yao kuhusu kutoridhishwa na kitendo cha
kucheleweshwa marejesho ya mkopo wa TADB.
Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.
Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw.
James Ihunyo ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wa bodi ya Skimu ya
Umwagiliaji ya Mkula kufuatia kuchelewesha kwa makusudi malipo ya mkopo
walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Akizungumza wakati wa mkutano wa
pamoja na wanachama wa Skimu hiyo, Bw. Ihunyo alisema kuwa uzembe wa
Bodi hiyo umepelekea kuchelewesha marejesho ya mkopo wa takribani
shilingi milioni 790.
Mkuu huyo wa wilaya aliongeza pia kitendo cha Bodi hiyo inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kupambana na umaskini nchini.
“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo
kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,”
Bw. Ihunyo alisema.
Bw. Ihunyo aliongeza kuwa
kuchelewesha kurudisha mikopo hiyo kunakosesha wakulima wengine
kuchelewa kupata fursa hizo za mikopo hiyo nafuu inayotolewa na TADB
ambayo imelenga kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa
uchumi na kupunguza umaskini.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Kamanda alisema kuwa
tangu wapatiwe mkopo huo, baadhi ya wakulima wa skimu hiyo wamekuwa
wakichelewesha kwa makusudi kurejesha mkopo huo licha ya jitahada za
kuwahimiza kurejesha mkopo huo.
Bw. Kamanda alisema kuwa vitendo hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya
“Mheshimiwa Rais anahimiza watu
kufanya kazi kwa bidii sasa vitendo hivi ni kukaidi maagizo hayo hivyo
kupingana na dhana ya hapa kazi tu inayochagiza kufanya kazi kwa bidii,”
alisema.
Bw. Kamanda aliongeza kuwa Benki
ya kilimo imejipanga kuhakikisha inatekeleza maelekezo ya serikali ya
kuwawezesha wakulima nchini kwa kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa
katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Mwakilishi huyo wa Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa TADB imedhamiria na kujizatiti
kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye
tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa
fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo
nchini.
“Tuna dira ya Kuwa benki ya
mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji
wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Post a Comment