Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Mb) Jenista Mhagama akutana na kufanya mazungumzo na
Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Ms. Maniza Zaman Ofisini kwake na
kuzungumzia masuala mtambuka juu ya kuboresha huduma za watoto Jijini
Dar es Salaam Agosti 3, 2017.
Waziri Jenista pamoja na masuala
mengine amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kwa
kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa Programu
ya Kitaifa ya Masuala ya Kijamii (National Frame -work Social
Protection) na mapitio ya utengenezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii
(Social Security Policy) na kueleza kuwa Serikali imeguswa na jitihada
za UNICEF kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika Nyanja hii.
Ms. Maniza amesema “UNICEF ina
mipango mbalimbali inayotaka kutekeleza kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzania mipango hiyo ni pamoja na kuboresha masuala ya Elimu kwa
watoto, Masuala ya Lishe, Watu Wenye Ulemavu, UKIMWI kwani huduma hizi
ni za msingi hivyo UNICEF itaangalia namna ya kutekeleza mipango hii
kwa Tanzania”.
“Tumeweza kuandaa makongamano na
majukwaa ya wahariri kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari, Viongozi wa
Dini kuhusu masuala ya watoto nchini Uganda na Brazil ambayo imefanikiwa
kwa asilimia 80 hivyo tunaamini Tanzania pia inaweza kuanzisha majukwaa
kama hayo katika kuboresha masuala ya watoto hapa nchi kwa kushirikiana
na UNICEF” alisisitiza Ms. Maniza.
Jenista amemuahidi Mwakilishi
Mkazi Ms. Maniza kuandaa mazungumzo ya pamoja kwa kushirikiana na Wizara
na sekta nyingine ili kuweza kuzungumzia masuala ya watoto na masuala
mengine mtambuka kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuboresha masuala ya
watoto hapa nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Waziri Mkuu
Dar es Salaam.
Agosti 3,2017
Post a Comment