Mwenyekiti mwenza wa Bill &
Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates akizungumza na waandishi wa
habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta
ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
………………………………
NA WAMJW –DAR ES SALAAM.
TAASISI ya Bill & Melinda
Gates imetoa dola za kimarekani shilingi milioni 15 ili kusaidia mpango
wa matumizi ya mfumo wa kielektroniki kuimarisha upatikanaji wa huduma
bora katika sekta ya afya nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
mwenza wa Taasisi hiyo ambaye ni tajiri wa Dunia Bill Gate katika
uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya afya
jijini Dar es salaam wakati alipotembelea nchini Tanzania.
“Mfumo huu utasaidia na kuleta
ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ,maamuzi kwa watendaji wa afya
nchini Tanzania katika kutoa na kuboresha huduma kwa wananchi wao”
alisema Bill Gate.
Aidha Bill Gate amesema kuwa mfumo
huo utasaidia kuimarisha na kuboresha matumizi sahihi ya takwimu na
kuleta matokeo sahihi katika kufuatilia sawa pamoja na taarifa za utoaji
wa chanjo.
Kwa upande wake Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
kuwa Serikali ya awamu ya tano imekua ikitilia mkazo na matokeo chanja
katika kuleta ufanisi katika sekta ya afya.
“Tukiwa na mifumo mizuri ya
kielektroniki tutaweza kujua dawa gani zimepelekwa katika kituo flani na
kiasi gani cha dozi na aina ya dozi wamepewa wagonjwa gani” alisema
Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
mfumo huo utaboresha upatikanaji na uhifadhi wa taarifa za wagonjwa
kirahisi tofauti bna zamani kwani mafaili mengi kwa sasa yanahifadhiwa
kwa uhakika na usalama zaidi.
Post a Comment