TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamishna Jenerali waJ eshi la
Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye, amefanya
mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi
hilo.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACF)
Bakari Mrisho, amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo, nafasi yake inachukuliwa
na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa
wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) James
John toka Makao Makuu.
Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro
Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa
wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Baraza
Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa Viwanja vya Ndege
Nchini, Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu,
nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa.
Kamishna Msaidizi (ACF) Fikiri
Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza nafasi iliyokuwa wazi
baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya
Moto.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani,
Mrakibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa
wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy
Shirima toka Makao Makuu.
Mrakibu Msaidizi (ASF) Fatma
Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya
Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro ambaye amehamishiwa Makao Makuu.
Uhamisho huo ni Mabadilikoya
kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika
kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Imetolewana;
KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA,
MAKAO MAKUU.
16 AGOSTI, 2017.
Post a Comment