Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (aliyevaa fulana ya kijani) akiwasili kwenye Banda la
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) lililopo kwenye Viwanja vya
Ngongo, mjini Lindi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (kushoto) akikaribishwa kwenye Banda la TADB na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kulia).
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea
Banda la TADB. Anayemtazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,
Bw. Francis Assenga (kushoto)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango (katikati) mara alipotembelea Banda la
Benki hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon
Migangala.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (kulia) akizungumza na mmoja ya wanufaika wa mikopo ya
TADB, Bibi Constancia Andrea (kushoto) kutoka Umoja Cashewnut Group.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (kulia) akizungumza na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB), na Mfuko wa Kusaidia Kilimo (PASS) alipotembelea
Banda la TADB. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mtendaji wa PASS, Bw.
Nicomed M. Bohay (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga (wapili kushoto). Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon Migangala (katikati) na Meneja Mikopo wa
TADB, Bw. Samuel Mshote (wapili kulia).
…………………….
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango amelitembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) wakati wa maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa
katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Akiwa katika Banda hilo Dkt. Mpango alionekana kuridhishwa na jitihada za Benki ya Kilimo katika kuchagiza mapinduzi ya kilimo.
Akimpokea Waziri Dkt. Mpango,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alimjulisha
Dkt. Mpango kuwa ndani ya Banda la TADB jumla ya washiriki 14
wanaonesha bidhaa na huduma zao kupitia Benki hiyo ikiwemo wakinamama na
vijana.
Post a Comment