Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji,
Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda akiongea na Vyombo vya Habari kuhusu
matokeo ya uchunguzi wa suala la utata wa uraia wa Ndugu Wallace John
Karia, ambaye ni mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania, TFF. Kutokana na pingamizi lililowekwa na Wakili Imani
Madega, mgombea mwingine wa nafasi hiyo.
…………………………..
Idara ya Uhamiaji
Tanzania, imemaliza utata juu ya uraia wa mgombea wa urais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, baada ya kusema ni raia halali
wa Tanzania tofauti na wengine wanavyosema.
Uhamiaji wamefikia
hatua hiyo baada ya Karia kuwekewa pingamizi na mgombea mwenzake, Imani
Madega ambaye alisema mgombea huyo si Mtanzania, bali ni Msomalia, hivyo
hana vigezo vya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika
Agosti 12, mwaka huu.
Msemaji Mkuu wa
Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, amesema: “Baada ya kupokea taarifa hiyo,
tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba Karia ni Mtanzania na wala si
Msomalia.
“Karia alizaliwa
hapa nchini ambapo mama yake ni Mtanzania wakati baba yake ni Msomalia.
Kutokana na msingi huo, Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya
kifungu 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo
la 2002 na kanuni zake.
“Wakati huohuo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi. Ni hitaji la kisheria chini ya kifungu cha 7(1), pale mtu anapokuwa na
uraia wa nchi mbili kuukana uraia wa nchi moja anapofikisha umri wa
miaka 18 hatua ambayo Karia aliitekeleza na kuthibitishwa ni raia wa
Tanzania kwa kuzaliwa.”
Post a Comment