Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza katika moja ya mikutano. |
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa ipo haja ya kuangalia
nijinsi gani watu wenye kipato duni na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu
wanaweza kufikiwa na kuelimishwa umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya.
Meya Mwita
amesema hayo jijini hapa leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wasiku mbili wa
wadau wa kujadili upatikanaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu sambamba na
ukiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma hizo kwa watu wenye kipato
cha chini.
Amefafanua kuwa
watu wenye kipato cha chini ,makundi mbalimbali wanashindwa kuwa na huduma hiyo
kutokana na kukosa uhamasishaji, elimu ya kutosha hivyo akashauri kuwa ni vyema
jambo hilo likazingatiwa kwenye maeneo yote.
“
Tunapozungumzia huduma bora za afya kwa wakazi wa jiji letu, tuliangalie pia eneo la gharama za utoaji wa huduma, namna tunavyoweza kuihamasisha
jamii kujiunga na bima ya afya ili kumsaidia na kumhakikishia mwananchi
kupata huduma hiyo pale anapozihitaji”
amesema Meya Mwita.
Ameongeza kuwa
kwakuwa jiji la Dar es Salaam linaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu ni muhimu
kuhakikisha nguvu kazi iliyopo jijini hapa ni ile watu wake wana afya njema.
Amesema jambo
la msingi katika majadiliano ya mkutano huo, ni kuainisha hatua zinazo hitajika
kuchukuliwa ili kuhakikisha wakazi wa jijini hapa ,hususani wale wenye kipato
cha chini na waishio kwenye mazingira magumu wanafikiwa na kupata huduma bora
za afya.
Hata hivyo alisema
kulingana na takwimu za sense ya Taifa ya mwaka 2012, jiji la Dar es Salaam
linakadiriwa kuwa na takribani watu milioni 4.4 hivyo kwa kuzingatia hilo ni
muhimu kuwa na mipango madhubuti ambayo itawawezesha wakazi wake kupata huduma
bora za kijamii, hususani za kiafya.
Jiji la Dar
es Salaam limekuwa na ushirikiano na urafiki wa jiji la Hamburg kwa kipindi cha
miaka 10, mkutano huo ni mwendelezo wa juhudi za wadau na Taasisi ndani ya
majiji haya katika kuendeleza utamaduni wa undugu na urafiki uliopo.
Mkutano huo
umehusisha , Tume ya Kikristu ya huduma za jamii (CSSC), marafiki kutoka
Diakonie ya Hamburg Ujerumani, Madiwani
kutoka kata za Mtoni Mtongani, Ukonga, Buguruni na zinginezo.
Post a Comment