Timu ya Ruvu shooting ya Mkoani
Pwani inayojulikana kama Leicester City jioni ya Leo itashuka kucheza
mchezo wa kirafiki na Matajiri wa Singida United mchezo unaotarajiwa
kupigwa katika dimba la Mabatini Mlandizi majira ya saa kumi 1:00
jioni.
Akizungumza na Mtandao wa mapema
asubuhi Leo msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire,amesema kuwa wamejipanga
vizuri na kitakuwa kipimo tosha kwao kuelekea msimu wa Ligi wa 2017-18
na wanaimani kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Leo tunataka kuweka historia ya
kushinda magoli mengi kwani tuna mabomu ya Nyuklia kama yale ya Korea
Kaskazini yanayoitisha dunia kwa sasa na sisi tuna full mziki kwani tuna
wachezaji wazuri tuliowasajili pamoja na hao wa zamani hivyo Singida
United watatafuta njia ya kutokea na tutawakaribisha kwa kipigo kabla ya
ligi kuanza’amesema Bwire
Hata hivyo Msemaji huyu amesema
kuwa Mchezo utakuwa mzuri kwani Singinda wanafundishwa na kocha bora
pamoja na kufanya usajili mzuri wa wachezaji wazoefu na michuano
mbalimbali hivyo wataleta upinzani kwao ila haiwezi kuwazuia kushindwa
kupata ushindi kwao.
Kwa upande wa Nahodha wa klabu ya
Singida United,Nizar Khalfani amesema kuwa mchezo huo wanaujukulia kwa
umakini zaidi na wanajua wanakutana na timu ya aina gani huku wakiwa na
kumbukumbu ya Kupoteza mchezo wao dhidi ya Lipuli FC ya mkoani Iringa.
“Tumejiandaa vizuri na wachezaji
wote wapo katika hali nzuri kwa maelekezo ya kocha Mkuu Hans Van Der
Pluijm,kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani kocha anaendelea kutafuta
kikosi cha kwanza ikizingatiwa wachezaji wengi ni wapya”Amesema Khalfani
Singida United imepanda msimu huu
na tayari imeanza kuonesha cheche kwa kufanya usajili mkubwa kwa
kuwanyakuwa wachezaji bora wenye uzoefu na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
bara pamoja na ukanda wa bara la Afrika kwani ina kocha bora mwenye
Rekodi Tanzania na Afrika akiwa na Yanga aliweza kutetea taji la Ligi
Kuu mara mbili na kuchukua kombe la FA na Ngao ya Hisani na akiwa nchini
Ghana aliipa mafanikio timu ya Berkmu Chelsea ambayo ilifika katika
hatua ya Ligi ya Mabingwa.
Singida United huu utakuwa mchezo
wa nne wa Kirafiki kucheza wakiwa wameshacheza na Pamba ya Mwanza na
kushinda magoli 5-0,Alliance School wakashinda 2-0 na kupoteza mchezo
mmoja dhidi ya Lipuli FC 1-0 na wanatarjia kucheza mechi moja siku ya
Jumamosi Agosti 5 dhidi ya Mabingwa wa Kihistoria Yanga na watasafiri
kwenda nje ya nchi kucheza michezo mbalimbali ya kujipima nguvu zaidi
kabla ya kuanza kipute cha Vodacom Ligi.
Post a Comment