MKURUGENZI Utawala na Uendeshaji
wa Hospitali ya Mnazimmoja Abubakar Khamis Hamadi akitoa maelezo ya
mafunzo yakuwajengea uwezo zaidi walinzi wanaolinda Hospitali, mafunzo
hayo yamefanyika Hospitali ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar
Harusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya siku moja kwa walinzi
wanaolinda Hospitali za Serekali na kuwataka wawe wakarim katika kutoa
huduma.
Baadhi ya walinzi katika mafunzo wakifuatilia hutuba ya NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said hayupo pichani.
NAIBU Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman katika picha ya pamoja na walinzi wanaolinda Hospitali za Serekali.
PICHA NA MAKAME MSHENGA.
………………………………………………………………………
Na Maryam Kidiko-Maelezo Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Afya Harusi
Said Suleiman amewataka Walinzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kubadilika
katika utendaji wa kazi zao ili kuongeza mashirikiano kati yao na
wananchi wanaokwenda kwa ajili ya kupata huduma mbali mbali katika
hospitali hiyo
Hayo aliyasema katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja kwenye Mafunzo ya Siku moja ya Walinzi wa Hospitali hiyo
ambayo yanalengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi zao na kuongeza
Mashirikiano na wateja wao.
Aliwaeleza walinzi hao kuwa
kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya walinzi wamekuwa wakitumia lugha
mbaya kwa wagonjwa na wananchi wanaofika kuangalia wagonjwa wao jambo
ambalo sio zuri.
Aliwasisitiza walinzi wa
Hospitali ya Mnazimmoja kutumia lugha nzuri kwa Wagojwa kwani kufanya
hivyo itapelekea kujenga mashirikiano katika utendaji mzima wa kazi
yao.
Alisema kunatofauti kubwa kati
ya ulinzi wa Hospitali na ulinzi katika sehemu nyengine kwani mara
nyingi wananchi wanaofika Hospitali wanahitaji kuhurumiwa kutokana na
mazingira wanayokuwa nayo.
“Walinzi wetu tunawaamini sana na
tunajuwa mnakumbana na changamoto nyingi lakini ni lazima mtumie akili
za ziada ili Wagojwa wanapofika wajiskie furaha hatakama wapo katika
huzuni,”Alisema Naibu Waziri.
Hata hivyo alishauri zinapotokea
Changamoto ndogo ndogo kuzishughulikia kwa njia nzuri za ushirikiano
kwa pande zote zinazohusika .
Aidha aliwaeleza walinzi hao kuwa
baada ya kupata mafunzo hayo Serikali haitawavumilia kuona wanaenda
kinyume na utaratibu uliowekwa katika kuwahudumia wananchi.
Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji
wa Hospitali ya Mnazimmoja Abubakar Khamis Hamadi alisema lengo la
mafunzo hayo ni kuongeza mashirikiano mazuri kati ya Wagojwa, wananchi
wanaofika kwa ajili ya kuangalia wagonjwa na Walinzi.
Alieleza matumaini yake kuwa
mafunzo hayo yatawawezesha Walinzi kujuwa njia sahihi za kuwashuhulikia
wateja wao wanapofika katika Hospitali na kujuwa wajibu wao.
“ Tunapata malalamiko mengi
kutoka kwa Wagojwa hivyo tumeamuwa kutowa mafunzo hayo kwa Walinzi ili
kuondoa matatizo na kuongeza mashirikiano mazuri baina yao,” alisema
Mkurugenzi huyo.
Aliwataka walinzi waliopata
mafunzo hayo kuyafanyia kazi ili kutimiza lengo la mafunzo yenyewe na
kuleta ufanisi katika kazi yao bila kutokea malalamiko mengine.
Mkurugenzi Abuubakar amewaomba
Wananchi wanaofika hospitalini hapo kutowa mashirikano mazuri kwa
Walinzi na iwapo litatokezea tatizo wafike katika kitengo cha huduma kwa
Mteja kwa lengo la kushughulikiwa.
Msaidizi Mkuu wa Walinzi
Aboubakar Hassan Bakari aliahidi baada ya mafunzo hayo watabadilika na
kuwashauri walinzi wenzake kuwa waadilifu huku wakijua wao ni kampuni ya
ulinzi ya Kibiashara hivyo wanatakiwa kuvutia waajiri wao.
Mmmoja wa Walinzi waliopata
mafunzo hayo Mwanaidi Mriha Nasibu alishukuru kupata mafunzo hayo ambayo
yatawasaidia kutatuwa Changamoto zilizopo baina yao na Wagojwa.
Post a Comment