NA CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,amelishukuru Shirika la
Maendeleo la Japani (JICA) kwa kukamilisha mradi wa Barabara na bustani
ya Kaburi moja iliyopo mtaa wa Samora jijini hapa.
Mradi
huo ambao ulianza utekelezaji wake Desemba mwaka jana na kusainiwa na
Meya Mwita ambapo leo baada ya kukamilika umekabidhiwa kwa halmashauri
ya manispaa ya Ilala leo (jana).
Meya Mwita
alieleza kuwa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 840 ikiwa
na malengo ya kuboresha mtaa wa samora ili kuwezesha magari kutembea kwa
uangalifu zaidi sambamba na kuliweka jiji kwenye muonekano mzuri.
Alisisitiza
kuwa mradi huo umechukua nafasi kubwa ya maeneo ya maegesho ya magari,
lakini umepelekea kuwa na muonekano mzuri kutokana na maboresho
yaliyofanyika.
Hata hivyo mwakili wa JICA
Nchini Tanzania Toshio Nagase alieleza kuwa mradi huo utawezesha
kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Mradi
huo wa barabara na bustani ya kaburi moja uliopo mtaa wa Samora,
ulisainiwa na halmashauri ya jiji na hivyo kukabidhiwa katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Post a Comment