Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

August 2017

1Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamisi Issa, mara alipowasili katika mkoa huo akiwa njiani kuelekea mkoa wa Arusha, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ili kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao


2Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili katika mkoa wa Kilimanjaro, akiwa njiani kuelekea mkoa wa Arusha, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ili kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao, kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamisi Issa.
3Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akizungumza na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ally Lugendo, na Mkuu wa chuo cha Polisi Moshi (CCP), SACP Ramadhan Mungi (kushoto), mara alipowasili katika mkoa wa Kilimanjaro, akiwa njiani kuelekea mkoa wa Arusha, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ili kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.
Picha na Jeshi la Polisi.

Lameck Ditto.

BAADA ya ngoma zake mbili alizotoa hivi karibuni kudaiwa kubuma, staa wa Wimbo wa Moyo Sukuma Damu, Lameck Ditto ‘Ditto’ amefunguka kuwa habari hizo siyo za kweli, kwani kwa upande wake anaona ziko vizuri.

Akichonga na Risasi Vibes, Ditto alisema ngoma zake hizo ambazo ni Bembea na Nabadilika hazijabuma kwani siku zote amekuwa akifanya muziki ambao umekuwa na mashabiki wengi kwa hiyo hauwezi kukwama kwenye vyombo vya habari ‘media’ hata siku moja.

“Nimeona kwenye mitandao ya kijamii watu wakidai nyimbo zangu nilizoachia hivi karibuni zimebuma, hilo si kweli maana kama ni video nimepeleka kwenye media mbalimbali na zinapigwa kwa hiyo watu waache kuzungumza vitu ambavyo havina ukweli ndani yake,” alisema Ditto.

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco anatarajiwa kuikosa mechi ya watani wa Jadi 'Ngao ya Jamii' inayochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kutokana na kutokuwa vizuri kiafya.

Hayo yamebainishwa na Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja wakati alipokuwa anazungumza na mashabiki zao kupitia mtandao wao na kusema wamejiandaa vizuri kuwapa raha mashabiki watakaojitokeza uwanja wa Taifa kutazama mtanange huo kwa kuwa wanakikosi kizuri kilichokamilika.

"Sisi kama Simba tunahitaji ushindi katika mechi ya leo kwa sababu itatusaidia kutuweka katika nafasi nzuri huko mbeleni. Wachezaji wote wako vizuri kasoro wawili ambaye ni John Raphael Bocco pamoja na Said Mohamed. Nawaomba mashabiki wa Simba waje kisimba kisimba kuipa ushirikiano timu yao iwapo uwanjani ili wachezaji waweze kufanya vizuri zaidi ya vile walivyopanga kufanya leo", alisema Mayanja.

Kwa upande wake, Nahodha wa Simba Method Mwanjali amesema wamejipanga vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo imekuwa yenye kutazamwa kwa jicho pana na mashabiki wao ili waweze kupata furaha ya ushindi.

Bonyeza Links Zifuatazo Kusoma zaidi na Kuapply

6 Jobs Opportunities at NMB Tanzania

Job Opportunity at Vodacom Tanzania

Job Opportunity at Qatar Airways, Reservation & Ticketing Supervisor

Job Opportunities at Mwananchi Communication Limited

Job Opportunity at Standard Bank, Officer, Credit Risk Management

Job Opportunity at Standard Bank, Officer, Accounts Payable

Job Opportunity at Palladium Group (Tanzania) Limited, Program Manager

Job Opportunity at Sunda Investment Co Limited, Customer Service Supervisor

Nafasi zaidi Ingia www.ajirayako.co.tz


Kiungo mpya wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

WAKATI kikosi cha Simba leo hii kikishuka uwanjani kupambana na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, kiungo mpya wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ameondolewa kwenye jukumu la kupiga penalti.

Niyonzima ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga kwa kitita cha Sh milioni 115, huenda asipige penalti kwenye mchezo wa leo, endapo hali hiyo itatokea.

Hali hiyo inatokana na kuonyesha uwezo wa chini wa kupiga penalti katika mazoezi ya juzi jioni na jana asubuhi ya timu hiyo ya kujiandaa na mechi hiyo Ngao ya Jamii yaliyofanyika katika Uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo, penalti zote alizopiga Niyonzima zilipanguliwa na makipa wa timu hiyo, Aishi Manula pamoja na Emmanuel Mseja.

Wachezaji wengine ambao katika mazoezi hayo walionyesha kiwango duni katika upigaji wa penalti walikuwa ni James Kotei, Method Mwanjale pamoja Laudit Mavugo.

Akizungumzia hali hiyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog alisema kuwa: “Mapungufu hayo nimeyaona lakini lakini nitahakikisha nayafanyia kazi ili wote kwa pamoja waweze kuondokana na tatizo hilo.

“Lakini ikitokea katika mechi yetu tukapigiana penalti na Yanga kuna wachezaji wengi wanaoweza kupiga na kutuwezesha kupata ushindi,” alisema Omog.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana Simba walishinda mabao 2-1, kwenye mchezo wa ligi kuu.


BENCHI la Ufundi la Yanga, limesema kuwa leo Jumatano linaanza kuhesabu makombe ya msimu wa 2017/18 kutokana na kuwa na uhakika wa kuifunga Simba.

Leo Jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  Yanga itapambana na Simba ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa msimu wa 2017/18.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten, amesema kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kisiwani Pemba, wana uhakika wa kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao, Simba.

“Mechi yetu na Simba tuna uhakika wa kushinda kutokana na maandalizi tuliyoyafanya, tumejiandaa tayari kwa kuanza kuhesabu makombe msimu wa 2017/18, hakuna mtu wa kuzuia jambo hilo.

“Benchi la ufundi chini ya kocha George Lwandamina, limetuhakikishia kwamba wachezaji wote waliokwenda kambini Pemba wapo vizuri kiafya tayari kucheza mechi hiyo, inafahamika tangu zamani kwamba Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya na Benno Kakolanya watakosekana kutokana na majeraha mbalimbali waliyonayo,” alisema Ten.


Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), jana ulibomoa nyumba tatu zilizopo Kimara Stop Over, jijini hapa ambazo ni kati ya 286 zilizowekewa kinga ya muda na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.

Hiyo ni sehemu ya operesheni ya kubomoa nyumba zaidi ya 1,300 zilizo ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya.

Wakati kazi ya kubomoa nyumba hizo ikiendelea, diwani wa zamani wa Saranga, Ephrahim Kinyafu alisema kinga ya muda kuzuia nyumba kubomolewa ilitolewa Agosti 18 baada ya wananchi 286 kwenda mahakamani na kwamba wamesikitishwa kuona zinabomolewa licha ya hati ya kuzuia kutolewa.

“Kwa uamuzi huu uliofanywa na Tanroads wa kubomoa hizi nyumba kwa kukaidi agizo la mahakama, tunajiuliza huu ndiyo utawala bora?” alihoji.

Kinyafu alisema walikwenda mahakamani kwa kuwa ndicho chombo chenye mamlaka ya kusimamia sheria.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika alisema uamuzi huo ni kinyume cha sheria na ameitaka Mahakama kuingilia kati na kuchukua hatua dhidi ya Tanroads.

Mhandisi wa wakala huyo Kimara, Johnson Rutechura alisema, “Hatuna taarifa juu ya nyumba ambazo zina kinga.”

Msimamizi huyo wa bomoabomoa alisema hawakupewa barua yoyote kutoka mahakamani hivyo hawatambui kama kuna nyumba zenye zuio.

Waliobomolewa

Kati ya nyumba hizo tatu, moja ni ya Nicomed Leo (61). Mbali ya nyumba hiyo, mzee huyo alikuwa na nyumba nne, mbili zikiwa za kawaida na nyingine za ghorofa. Iliyobomolewa na Tanroads ni ya kawaida iliyokuwa karibu zaidi na barabara.

“Nilikuwa na kinga ya mahakama, niliibandika getini lakini nashangaa wamebomoa hapa haki iko wapi,” alisema na kuongeza kuwa baada ya kupata kinga, aliamini atakuwa salama lakini alishangaa jana asubuhi kuona akipigiwa simu kwamba nyumba yake inabomolewa.

“Nilijua wananitania, lakini nilipofika hapa nikakuta kweli wanabomoa na nilibandika karatasi za kinga getini na ukuta wa nyumba,” alisema.

Kutokana na tukio hilo, Leo, ambaye baada ya nyumba zake kuwekewa alama ya X alihojiwa na waandishi wetu na kusema “Nimeshajiandaa kisaikolojia hata wakija kubomoa mimi nitajenga kibanda hapahapa maana sina pakwenda,” jana alisema amekosa amani na hana imani tena hivyo ameamua kubomoa mwenyewe.

“Wanataka kuniua kabla ya wakati,” alisema huku akitetemeka na jasho likimtiririka usoni. Mzee huyo ambaye katika mahojiano ya awali alisema nyumba zake zilikuwa na thamani ya Sh900 milioni hakuwa na hamu ya kuzungumza na wanahabari kwani walipojaribu kumhoji aliwaambia kwa kifupi, “Mtanisaidia nini hata nikisema zaidi ni kama nachochea tu nyumba yangu kubomolewa naomba mniache.”

Ijumaa iliyopita, Leo alizirai baada ya kushuhudia nyumba ya jirani yake ikibomolewa. Inaelezwa kwamba alijaribu bila mafanikio kuwaomba maofisa wa Tanroads wasibomoe nyumba yake lakini ilishindikana ndipo alipoanguka. Kuona hivyo, maofisa hao waliahirisha kubomoa nyumba hiyo lakini wakiahidi kurejea jana.

Mwingine aliyebomolewa nyumba yake huku kukiwa na zuio la Mahakama ni Aisha Juma ambaye alisema walichokifanya ni kuokoa vitu vichache vya ndani.

Aisha alisema wanachosubiri sasa ni kusikia mahakama itasemaje tena baada ya tukio hilo.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Siro, amejibu tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa na kuwaonea viongozi wa vyama vya upinzani, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu juu ya hilo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, IGP Sirro amesema jeshi la polisi halimkamati mtu kwa sababu ni kiongozi wa chama cha siasa au ni kiongozi wa dini, bali humkamata mtu iwapo kuna taarifa za uhalifu zilizowafikia kwani halifuati siasa., hivyo jukumu lao ni kuhakikisha usalama wa nchi.

“Polisi hakamati viongozi wa siasa, polisi hakamati viongozi wa dini, polisi anakamata mhalifu, na mhalifu anapomkamata anamhoji kama kuna ushahidi anampeleka mahakamani, kama hakuna ushahidi anamuachia”, alisema IGP Sirro.

IGP Sirro aliendelea kwa kuwataka wananchi wamuache afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayewajibika na kusimamia amani, na kusema endapo utakamatwa na kukutwa hauna hatia, hawatasita kukuchia huru.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi amesema mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu tosha ya kunyang'anywa ardhi hiyo pamoja na kufutiwa hati ya umiliki kwa kuwa anaingizia hasara serikali

Waziri Lukuvi amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja tokea kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Mh. Fredrick Sumaye kudai chanzo cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM na kwenda kuupa nguvu upinzani.

Akiongea kuhusu mashamba na viwanja kuchukuliwa Waziri Lukuvi amesema,
"Kila mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya ardhi ni sababu tosha ya wewe kunyang'anywa shamba lako au ardhi unayomiliki".

Akiendelea kuongea Waziri Lukuvi amesema
"Imejitokeza kwa watu wachache kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi kuliko hata uwiano wa uendelezaji wa ardhi hiyo, kwa mfano kuna hati moja hapa ambayo inapigiwa kelele tokea mwaka 1939 imekuwa ikitembea mikono mwa watu. Sasa miaka ile watu walikuwa wachache unapokwenda kuchukua ardhi ya kijiji hekari elfu 60 kwa mfano hivi sasa wananchi utakuwa umewaachia kitu gani?"

Pia Waziri Lukuvi amesema imekuwa kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi maeneo  huwa wanakimbilia kuchukua sehemu zenye manufaa makubwa kwa upande wao na mwishowe wanashindwa kuendelezaa maeneo hayo kama walivyoyakimbilia.

"Unawahi kuchukua sehemu zenye manufaa kama mto, ardhi inayolimika, sasa unachukua hekari zote hizo halafu huliendelezi mwishowe shamba hilo hilo tunalikuta Benki umelikopea fedha. Kisha umepata fedha hizo unakwenda kujengea 'apartment' sehemu nyingine na kule wananchi wanalimezea mate.Serikali wanatumia nguvu kubwa sana kutuliza wananchi wasivamie hilo shamba , halilimwi, serikali hatupati kodi", alisisitiza Lukuvi.

Kwa upande mwingine, Waziri Lukuvi amesema serikali imekuwa na huruma kwa miaka mingi kwa wananchi wake lakini serikali ya uongozi huu wamekubaliana kila mtu afuate sheria anazo paswa kuzifuata.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetiliana saini na Kampuni ya Thades ya Ufaransa kuhusu mkataba wa ufungaji wa mitambo ya rada nne za kuongozea ndege ambazo zitawezesha kuongeza mapato ya nchi kwa kuruhusu ndege kubwa zaidi kutua na anga lote la Tanzania litaonekana.

Hivi sasa Tanzania ina rada moja ya kuongozea ndege iliyonunuliwa mwaka 2002 ambayo uwezo wake umepungua kutokana na mabadiliko yanayotokea kwa haraka katika sekta ya usafiri wa anga.

Mradi huo utagharimu Sh bilioni 61.3 utachukua kipindi cha miezi 18 kukamilika, kufungwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA) na Uwanja wa Ndege Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (pichani) alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji saini huo ambao ulienda sanjali na uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA.

Profesa Mbarawa alisema mradi huo, pia utaiwezesha Tanzania kuboresha utoaji wa huduma za kuongoza ndege, kukuza sekta ya usafiri wa anga na hatimaye kuongeza mchango katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Mradi huu ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Serikali ya Rais John Magufuli inayodhihirisha nia ya kuimarisha sekta ya usafiri wa anga na kufikia azma ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025,” alieleza Profesa Mbarawa.

Kwa mujibu wake, mchakato huo ulianza muda mrefu, naye aliukuta akaamua kuchukua jukumu hilo kwa uaminifu mkubwa kwani jambo hilo halikuwa rahisi hata kidogo. Alielezea faida ya kuwekwa rada hizo zitawezesha ndege nyingi kupita katika anga la Tanzania kwa kuwa litakuwa ni salama hivyo kuiwezesha serikali kupata mapato, pia katika sekta ya utalii kutakuwa na mapato mengi kwa kuwa ndege kubwa zitaleta watalii nchini.

“Kwenye migodi zinaingia ndege nyingi na kwenye mbuga za wanyama, lakini tumeshindwa kuziona, lakini baada ya kuwekwa rada hizi tutaziona na kuwasiliana na TRA ili kuhakikisha tunapata mapato sahihi,” alisema.

Alisema hivi sasa ndege zinazoruka urefu wa futi 24,500 anga la Tanzania hawazioni, rada za Kenya ndizo zinaziongoza, lakini hizi zikishafungwa hali hiyo itatengemaa. Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema mradi huo ni miongoni mwa mipango mikakati iliyopewa kipaumbele cha juu na mamlaka hiyo katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 kwa lengo la kuimarisha uwezo wa Tanzania katika kutoa huduma za kuongoza ndege, kuboresha usalama wa sekta ya usafiri wa anga pamoja na kuongeza mapato yatokanayo na tozo ya huduma za kuongozea ndege.

Alisema ongezeko la ndege zinazotumia anga la Tanzania limesababisha kuwa na mahitaji ya mitambo ya aina hiyo ili kufanikisha taratibu za urukaji ndege kwa kufuata viwango vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

“Kutokana na uwezo wa rada yetu kupungua baadhi ya nchi jirani zilikuwa zimeanza kampeni za kutaka kukasimiwa anga la Tanzania ili kuliongoza, kutokana na kuwa na rada zenye uwezo mkubwa ambazo zilikuwa zinaweza kumulika hata anga la Tanzania,” alisema Johari na kuongeza kuwa jitihada za kuwa na rada mpya za kuongoza ndege zilianza miaka mitatu iliyopita ambapo maombi hayo yalikuwa yakiwasilishwa Serikali Kuu.


Kama ukinywa damu kasi kidogo sana (labda vijiko vichache vya chai), na iwapo damu hiyo haina vijidudu vya bakteria au virusi vya magonjwa, basi damu hiyo yaweza isiwe na madhara kiafya. Kama damu hiyo ni nyingi na pia huna hakika kuhusu usalama wake dhidi ya vijidudu, usinywe.

Jambo la ajabu ni kwamba, damu unapoinywa ni sumu. Kama damu ikiwa kwenye viungo vinavyohitaji damu — kama moyo, mishipa ya damu na vingine — inakuwa na umuhimu mkubwa kwa kiumbe hai. Lakini ikinywewa inakuwa ni hadithi tofauti kabisa. Inabidi ieleweke kwamba kila sumu inahitaji dozi fulani iweze kuonesha madhara yake, ni sawa na kwamba unaweza usidhurike utakapokunywa tone moja la sumu lakini unapoongeza kiasi, hatari inakuwa kubwa zaidi.

Kwa sababu damu ina kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma — na kwa sababu mwili unapata tabu kutoa madini ya chuma yaliyozidi — mnyama yeyote anayekunywa damu mara kwa mara anakuwa kwenye hatari ya kuwa na kiasi kikubwa cha madini haya. Ingawa madini ya chuma ni muhimu sana kwa wanyama wote (na kwa kila kiumbe hai), yanapozidi huwa ni sumu inayoweza kusababisha magonjwa kama magonjwa kama homa ya ini (aina B na C), mapafu kujaa maji, kupungua kwa maji mwilini, shinikizo la chini la damu, matatizo ya mfumo wa fahamu, magonjwa mbalimbali ya zinaa pamoja na UKIMWI.

Tofauti na binadamu, miili ya wanyama ina uwezo wa kumeng’enya damu kwakuwa ina mfumo maalum wa kuwezesha kazi hii. Wanyama wanaokunywa damu wanahitaji kiasi kikubwa cha madini ya chuma yanayomsaidia kutengeneza sukari inayobeba hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye tishu mbalimbali za mwili.

Kwa wanyama kama popo, damu wanayokunywa inakuwa nyingi kuliko inayohitajika mwilini, kwahiyo kuna mfumo maalum wa kuitoa. Wanapoinywa, damu inapita kwenye njia maalum inayonyonywa virutubisho. Tafiti zimeonesha kwamba mfumo huu una ukuta wa majimaji kwenye utumbo ambayo ina uwezo wa kuzuia madini ya chuma yasiingie kwa kiasi kikubwa kwenye mfumo wa damu.

Sisi binadamu si kama popo kwa sababu hatuna mfumo wa kusaidia kudhibiti kiwango cha madini ya chuma kinachoingia mwilini, kwahiyo damu itatuua.

Kama ukipata jeraha dogo la kuchanika midomo na kwa bahati mbaya ukanywa kiasi cha vijiko vichache vya damu yako au iwe unapenda kunywa damu za wanyama kama ng’ombe, mbuzi au kondoo wanapochinjwa, ni bora ukajua madhara ya kiafya yanayotokana na kunywa damu hiyo hata kama ni kiasi kidogo. Yawezekana ni muhimu sana kutufanya tuwe hai ikisukumwa na moyo au kupita kwenye mishipa ya damu lakini itakuchukua uhai huo kama ambavyo sumu yoyote ile itavyofanya utakapokuwa na tabia ya kuinywa mara kwa mara.


Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, atalazimika kufanyia kazi zake akiwa nyumbani baada ya panya kuharibu ofisi yake iliyopo Ikulu.

Msemaji wa Rais Buhari, Garba Shehu, amesema, panya hao wameharibu samani za viyoyozi katika ofisi hiyo hivyo kiongozi huyo hawezi kufanya kazi katika ofisi mbovu ambayo itakarabatiwa kwa kipindi cha miezi mitatu.

Bw. Garba amesema, hatua ya Rais Buhari kufanyia kazi zake nyumbani hakutaathiri ufanisi wake kwa aina yoyote ile.

Rais Buhari alirejea nyumbani Nigeria Jumamosi iliyopita baada ya kukaa Jijini London nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 100 alikokuwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa ambao hata hivyo haujawekwa wazi.

Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu.

Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba.

1.Mama anapokuwa na matatizo  uvimbe (fibroid),  huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara.

2. Uzito mkubwa (unene)
Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda.

3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara
Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika.

4. Utoaji mimba
Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba.

5. Matumizi ya Pombe,Sigara
Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo.

6. Magonjwa sugu
Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.


Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.

Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.

Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO 
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.

Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers' Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.

Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.

Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.

Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.

Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.

Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.

Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO 
Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili.
Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:-

Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa.

Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.


  1. Kushindwa kumeza vizuri chakula. 
  2. Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni. 
  3. Kujisikia vibaya baada ya kula. 
  4. Kupungua uzito. 
  5. Kukosa hamu ya kula. 
  6. Kutapika damu. 
  7. Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito. 
  8. Kichefuchefu & kutapika. 


JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-
Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteka wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :- 

Kupima damu 'Blood test' 
Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

Kupima pumzi 'Breath test'
Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test' 
Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi.  Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray' 
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO 
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole.

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.

Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine,    hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo.

H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

Wafanyikazi sita wa baraza la mji wa Ntugumo nchini Uganda wamesimamishwa kazi kwa madai ya kutovaa tai.

Kulingana na gazeti la Daily Nation, walisimamishwa kazi na afisa mkuu Kweyamba Ruhemba ambaye aliwapata na makosa ya sheria za baraza hilo kwa kuvaa mavazi kwa njia ambayo inatoa picha mbaya kwa wilaya hiyo.

Wote walipatikana bila ya tai.


Gazeti hilo limemnukuu Ruhemba akisema kuwa maafisa hao wamesimamishwa kazi kwa miezi miwili ili kuwafunza kuvaa kwa heshima.

Mapema 2017, wizara ya nguvu kazi ilitoa maelezo ikipiga marufuku nguo zinazoonesha ndani, zile za kubana kwa maafisa wasiovaa sare za kazi miongoni mwa wafanyikazi wa serikali.

Kulingana na gazeti hilo katibu wa wizara ya utumishi wa umma , bi Catherine Bitarakwate Musingwiire alisema kuwa maelezo hayo yanaenda sambamba na sheria za wizara ya utumishi wa umma.

Sheria ya utumishi wa umma nchini Uganda , ya mwaka 2010 inasema uwa maafisa watalazimika kuvaa kwa heshima kulingana na viwango vinavyokubalika katika jamii ya Uganda.

Gazeti la Daily Nationa linasena kuwa sheria hiyo hatahivyo imenyamaza kuhusu ni nini kitadhihirisha kwamba mtu amevaa kwa heshima ili kukubalika.

Katika sheria hiyo wafanyikazi wanawake wanahitajika kuvaa sketi ama rinda ambalo halipiti juu ya magoti na shati yenye heshima.

Marinda ama tisheti zinazoonyesha ndani , marinda ya kubana, sketi fupi, viatu vya chini na nywele zilizopakwa rangi vimepigwa marufuku

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget