Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MIZANI 94 YATAKIWA KUFANYIWA MAREKEBISHO WILAYANI RUANGWA


Image result for picha ya mzani



Wakala wa Vipimo Mkoa wa Lindi imezuia matumizi ya mizani 94ya vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) katika Wilaya ya Ruangwa. Mizani hiyoimezuiwaisitumike katika msimu ujao wa ununuzi wa ufuta/korosho mpaka itakapofanyiwa marekebisho na Mafundi Mizani kwa kurekebisha mapungufu yaliyoainishwa na Wakaguzi wa mizani hiyo,ambapo Mizani hiyo itakaguliwatena na Maafisa vipimo mara baada ya matengenezokukamilika na endapo Mizani hiyo itakidhivigezoitagongwamuhuri  na kubandikwa stika maalum ndipozitaruhusiwa kutumika wakati wa msimu.

Katika zoezi la ukaguzi wa Mizani kwenye Wilaya ya Ruangwa Wakala wa Vipimo imehakiki jumla ya vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) 23 na kukagua jumla ya mizani 150 ambapo kati ya mizani hiyo iliyopimwa na kuhakikiwa kuwa sahihi ni mizani 56 na iliyozuiliwa kutumika mpaka itakapofanyiwa marekebisho ni mizani 94.
Mizani mingi imeonekana kuwa na mapungufu (haipimi sahihi) kwakuwa ilibainika baadhi ya mizani ina mapungufu kuanzia 200g hadi 1kg ambayo kwa kawaida mzani unatakiwa kuwa na Upungufu unaokubalika wa kiasi cha 80g tu. Vilevile baadhi ya mizani imechakaa na kupelekeakupoteza usahihi katika Upimaji wake kutokana na namna mizani hiyo inavyohifadhiwa kwani huifadhiwa katika maeneo machafu yenye vumbiambayo husababisha mizani kupata kutu, pia njia inayotumikakusafirishia mizani hiyo sisalama kwani mizani husafirishwa kwa Usafiri wa pikipiki ambao husababisha mzani kuangusha baadhi ya vifaa vyakemuhimu.
Meneja wa Mkoa Wakala wa Vipimo Lindi Bw. Stephen Masaweameeleza kuwa “tumeamua kuendeshea zoezi hili la ukaguzi wa mizani ili kubaini mizani iliyo sahihi na kuipitisha na kwaile itakayohitaji marekebisho mafundi watapitakuifanyiaukarabatikishatutaihakiki upya na kama itakuwa sawa tutaipitisha.
 Zoezi hili litapunguzasana gharama za uendeshaji wa vyama vya ushirika vya msingi kwani awali mafundi mizani walikuwa wanapita na kurekebisha mizani zote, hii ilikuwa inapelekea nyama vya ushirika vya msingi kutumia gharama kubwa ya matengenezo hadi Tsh. 400,000= kwa mzani Mmoja lakini kwa sasa mafundi watapita kurekebisha mizani iliyobainika kuwa na mapungufu ambayo yameainishwa na Wakaguzi wa mizani tu.”
Masawealisema, zoezi hili la ukaguzi wa mizani (kapani) ya vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) lilianzia katika Wilaya ya Ruangwa nasasa zoezi hilo linafanyika katika Wilaya ya Nachingwea.zoezihili la ukaguzi wa Mizani ni endelevu na litafanyika pia katika Wilaya zilizobakia ambazo ni Wilaya zaLiwale, Kilwa, Lindi Mjini na Lindi Vijijini kwa kuhakiki mizani zote za vyama vya ushirika vya msingi.
Pia, baadhi ya wananchi wameipongeza sana Wakala wa Vipimo kwa kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya Vipimo pamoja na kufanya ukaguzi wa Mizani kabla ya mafundi kupewa tenda ya kuitengeneza na Halmashauri, Miongoni mwao ni ndugu Laurent Adrian Muyaambae ni mwanakijiji wa Michenga A na ni karanimpimaji kwenye ghala la Michenga A.
Wakala wa Vipimo inatoawito kwa wakulima wote wa ufuta na Korosho kuhakikisha kuwa wanauza mazao yao katika vituo vyenye mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo na kupigwachapa ya bibi na bwana na kuweka tarakimu mbili za mwaka husika (17) kwa mwaka huu, na tumeanza kuweka stika maalum ya Wakala wa Vipimo mbele ya mizani yote iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo. Pia wahakikishe kuwa wanasoma kilo za mazao yaopindiwanapoenda kupima katika maghala na si kwa kumuaminikarani tu akishakusomea kwani wengine husoma kilo pungufu kwa ajili ya kuwapunja mazao yao.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget