Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

“Wanaocheza mchezo wa Drafti wasizarauliwe ,” Meya Mwita”

Meya wa jiji la Dar es salaam Isya Mwita aliye vaa kofia nyeupe akicheza Bao na mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah Mtolea aliye vaa shati  la maua, katika mchezo huo wa ufunguzi  Mchezo ambapo Meya alishinda mchezo mmoja na miwili wakatoka  suluhu
Washiriki wa mchezo wa Drafti wakiendelea na mchezo.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdala Mtolea akicheza mchezo wa Drafti na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita


NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya  wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewaomba wadau wamichezo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwakuwa ni michezo kama ilivyo michezo mingine.

Meya Mwita aliyasema hayo jiji hapa leo katika uzindua wa mashindano ya mchezo wa Drafti yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe yanga, halmashauri ya Temeke.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Meya wa jiji Mwita , yalihudhuriwa pia na Mbunge wa jimbo la Temeke Abdala  Mtolea , Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Drafti ambapo jumla ya washiriki 64 walishiriki.

Meya Mwita alisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini umekuwa ukizaraulika na kuonekana kwamba wanaoshiriki mchezo huo niwatu ambao hawana kazi za kufanya.

Alisema wapo wadau wengi ambao wanatoa vipaumbele kwenye michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete na michezo mingine huku wakiusahau mchezo huo , jambo ambalo linaonyesha kuwatenga makundi ambayo wamejikita kwenye mchezo huo.

Alisema “ Niwaeleze tu kwamba, huu mchezo ni mchezo mzuri kama ilivyo michezo mingine, leo hii wanaocheza mchezo huu wanazaraulika na kuonekana kwamba niwatu ambao hawana kazi, wasiojua kujishugulisha, jambo ambalo sio kweli natamani  mchezo huu ufahamika kama michezo mingine.

“ Kama kweli tukiunga mkono mchezo huu, ipo siku tutajenga majina yetu kupitia mchezo huu kama ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu, mpira wa pete, na hata mataifa ya nje yakatuunga mkono kupitia huu mchezo” aliongeza.

Aidha Meya Mwita katika hatua nyingine alisema kwamba ataunga mkono chama cha mchezo huo ili waweze kukisajili na kutambulika rasmi.

Aliongeza kuwa katika mashindano mengine , baada ya kusajiliwa kwa chama hicho, yatakutanisha kila halmashauri iliyopo jijini hapa na hivyo kupata mshindi kutoka kwenye halmshauri husika.

“ Jiji lina halmashauri tano, nataka kwenye mashindano mengine ambayo tayari chama hiki kitakuwa kimesajiliwa , kila halmashauri itashiriki, na mshindi atapatikana kutoka kwenye halmashauri nasio mmoja mmoja kama ambavyo tumefanya leo, ila huu ni mwanzo.

Hata hivyo Meya Mwita ameahidi katika mashindano yajayo kugharimia nauri na chakula kwa wachezaji watakao shiriki mashindano hayo na kuwa himzi wachezaji hao kuuthamini mchezo huo.


Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Meya wa jiji , Mwenyeiti wa Chama cha  mchezo wa huo mkoa wa Dar es salaam , Kiraba Ngibombi amesema chama kinakabiliwa na changamo nyingi  ikiwemo ukosefu wa ofisi na fedha za kuhudumia na kufanya usajili wa  chama hicho.

Mwenyekiti huyo amemuomba Mstahiki Meya katika mashindano yajayo kuwagharimia wachezaji chakula  na pamoja na nauri kwa ajili ya   wachezaji hao.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget