Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WALIMU WA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) NA VYUO BINAFSI VYA AFYA WAANDALIWA MAFUNZO YA MAADILI

unnamed
Kaimu Naibu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Bi. Amina Abdulkadir akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kufungua warsha ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli hiyo na viongozi wa wauguzi wa Hospitali za Serikali na Binafsi huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
A
Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisisitiza maadili kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya wakati akifungua warsha ya siku nne ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi katika skuli hiyo iliopo Mbweni.
A 1
Baadhi ya washiriki wa warsha ya maadili na utafiti  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo inayofanyika Skuli ya afya na Sayansi za tiba Mbweni.
A 2
 Mkuu wa Idara ya Uuguzi Mwanaisha Juma Fakih  akisoma malengo makuu ya warsha hiyo inayowashirikisha walimu wa Skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi wa hospitali za serikali na hospitali binafasi Mbweni.
A 3
Kaimu Mkuu wa Skuli ya afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Salum Seif akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo katika skuli hiyo iliyopo Mbweni.
A 4
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya (wa kati kati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya maadili na utafiti inayofanyika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ameiagiza Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kufanya tafiti kujua chanzo cha mmongonyoko wa maadili kwa wafanyakazi wa afya wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.

Alishauri baada ya kupata majibu ya tafiti hizo kuishauri serikali hatua ya kuchukuliwa ili kuinusuru hadhi ya taaluma ya afya ambayo inajengeka katika misingi ya ukarimu na kutoa huduma bila upendeleo.

 Naibu Waziri ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku nne juu ya Maadili na Utafiti kwa wakufunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na viongozi wa wauguzi wa Hospitali binafsi na Serikali  katika skuli hiyo  iliopo Mbweni.

Alisema watendaji wa Hospitali na vituo vya afya na hasa vya Serikali baadhi yao wanakiuka maadili ya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha mbaya
Alisema tatizo la unyanyasaji wagonjwa limekuwa kubwa zaidi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo ni tegemeo kubwa la wananchi wa Zanaizbar.

Aliongeza kuwa jambo la kusikitisha ni kuwa wafanyakazi wa hospitali za serikali ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa kukiuka maadili wanapokuwa katika vituo binafsi wanakuwa ni mfano wa kuigwa kwa tabia njema.

Hata hivyo Bi. Harusi aliwataka walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba kuwa mfano bora wa maadili na kuimarisha somo hilo kwa wanafunzi wao ili kurudisha hadhi ya taaluma ya afya na wananchi waendelee kuwaamini.

Kaimu mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Dkt. Salum Seif alisema somo la maadli ni moja kati ya masomo yanayopewa kipaumbele katika skuli hiyo lakini kupata elimu ni jamabo moja na kuitumia elimu uliyonayo ni jambo jengine.  
 Alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa watakuwa waangalifu na kuongeza udadisi katika sulala la maadili kwa wanafunzi wanaomba kujiunga na Skuli hiyo na atakaeonekana hawezi kukidhi kigenzo watamuacha.

Alisema tatizo kubwa linalochangia ukosefu wa maadili Zanzibar ni watu kuoneana muhali kutokana na kujuana sana na kupelekea kuzifumbia macho sheria zilizop
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget