Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO YATOLEA UFAFANUZI HOJA YA MBUNGE WA UBUNGO MHE.KUBENEA KUHUSU KUKABIDHIWA UWANJA WA TAIFA


Uwanja
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inapenda kutolea ufafanuzi hoja ya Mbunge wa Ubungo Mhe. Saed Kubenea kuhusu kukabidhiwa Uwanja wa Taifa ukiwa haujakamilika.
Ukweli ni kwamba Uwanja wa Taifa umejengwa kulingana na usanifu (design) wake kwa kufuata vigezo vya FIFA na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) na kukamilika ambapo vyombo vyote vya serikali vilikagua na kujiridhisha kulingana na makubaliano ya mkandarasi.
Uwanja wa Taifa umejengwa kwa mtindo wa kipepeo hivyo wakati wa mvua hususani yenye upepo mkali hupelekea maji kufika katika maeneo ya majukwaa likiwemo jukwaa kuu (VVIP) na sio kuwa uwanja huo unavuja.
Ujenzi wa Uwanja huo uligharimu kiasi cha shilingi Bilioni 56 mpaka kukamilika kwake.
Hata hivyo Wizara kwa kushirikiana na mshauri mwelekezi wamekubaliana kuweka paa eneo la jukwaa kuu (VVIP) ili kuepusha maji kuingia katika eneo hilo kipindi cha mvua.

Imetolewa na:


Genofeva  Matemu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
09/05/2017
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget