Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

TAMKO LA KLABU YA YANGA BAADA YA MANJI KUACHIA NGAZI




Baada ya taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kueleza kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji ameachia ngazi kuiongoza Yanga, tamko rasmi limetolewa juu ya ukweli wa suala hilo.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ametoa tamko kwa kusema kuwa hajapata taarifa rasmi juu ya ukweli wa suala hilo lakini amethibitisha kuwa bado hajawasiliana na Manji kama kweli amechukua uamuzi huo.
Akizungumza juu ya taarifa hizo, Mkwasa amesema: “Sijapata taarifa hizo rasmi, mimi ndiyo mtendaji mkuu wa klabu, bado sijakabidhiwa barua kwa kuwa sifanyi kazi kwa kutumia mitandao.

“Tunajua kuwa mitandaoni kuna taarifa nyingi ambazo siyo za kweli na zipo nyingine ambazo zimesababisha baadhi ya wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hivyo nasubiri kuona kama ni kweli, basi nitapatiwa barua rasmi na nitatoa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo.”
Alipoulizwa kama amewasiliana na Manji hivi karibuni, alisema: “Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa njia ya barua pepe kwa masuala ya kiofisi lakini sijakutana naye siku mbili hizi.”
Tangu mapema leo Jumanne kumekuwa kukisambaa barua ambayo inaonekana imesainiwa na mwenyekiti huyo akielezea uamuzi wake wa kutangaza kujiuzulu.
Barua yenyewe inayosambaa hii hapa:
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget