Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

PEMBA:WAJASILIMALI WATAKIWA KUZITAMBUA NA KUZIENDELEZA FURSA ZA BIASHARA


nm
Na  Masanja Mabula –Pemba .
 
WAJASIRIAMALI kisiwani Pemba wametakiwa kuzitambua na kuziendea fursa za kibiashara ili kufanya biashara yenye tija kwa lengo la kujiletea maendeleo pamoja na taifa kwa ujumla.
 
Wito huo umetolewa na Meneja wa urasimishaji rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania Makame Juma Pandu huko micheweni, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 
“Kuzitambua fursa za kiuchumi na kuziendea na kufahamu changamoto za kibiashara kutamfanya mfanyabiashara afanye biashara kwa uhakika na ataweza kujikwamua kiuchumi yeye binafsi na Taifa kwa ujumla” .Amesema meneja huyo.
 
Ameongeza kua baadhi ya wafanyabiashara wanashindwa kutenganisha biashara na mali  zao sambamba na kushindwa kutunza kumbukumbu sahihi za biashara zao hivyo kupelekea kufilisika kutokana na ufahamu mdogo wa biashara.
 
Nae Mkuu wa Idara ya bishara Pemba Ali Suleiman Abeid amewaomba wafanyabiashara hao kuacha kufanya biashara kimazoea na badala yake watafute elimu ya biashara ili wafanye biashara itakayowakomboa kiuchumi.
 
Kwa upande wake mratibu wa Mafunzo hayo Zuwena Abdalla Hilali amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo wadogo ili wafanyebiashara endelevu na yenye tija kwao na taifa.
 
Ameongeza pia mafunzo hayo yatawaelimisha wafanyabiashara hao umuhimu wa  kutumia taasisi za fedha ikiwemo mabenki kwa ajili ya kutunza fedha zao badala ya kutunza fedha majumbani.
 
Mafunzo hayo ya siku nne ni muendelezo wa mafunzo yanayotolewa na MKURABITA  kwa wafanyabiashara hapa nchini unahusisha wajasiriamali 50 kutoka Wilaya ya Micheweni.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget