Na Daudi Manongi.
Serikali kupitia Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa inategemea
kusambaza vifuko maalum vya kujifungulia vyenye vifaa vya kujifungulia
kwa wanawake 500,000 ambavyo vitasambazwa nchi nzima kulingana na
uhitaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Mhe.Dk Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini
Dodoma.
“Sera ya Afya ya mwaka 2007
inaeleza kuwa Huduma za kina Mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote
zinapaswa kutolewa bila malipo”,Alisisitiza Mhe.Kigwangala
Aidha amesema kuwa Serikali
haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji
na hivyo huduma hizo zitaendelea kutolewa katika ngazi zote katika vituo
vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za Serikali.
Aidha kwa upande mwingine
Mhe,Kigwangala ametoa rai kwa Wabunge kusaidia kusimamia utekelezaji wa
Sera walizokubaliana katika katika maeneo yao husika ili kuhakikisha
huduma hizi za kina mama zinapatikana kwa Gharama za Serikali kama
ilivyopangwa.
“Ili azma ya Serikali ya
Kuhakikisha akina mama wajawazito wanapata huduma nzuri na lengo la
kupunguza vifo vya mama na watoto inafanikiwa ni lazima usimamizi uwe wa
karibu sana”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
Aidha jumla ya kina mama 1,900,000
hujifungua kila mwaka nchini na kumekuwa na changamoto katika
upatikanaji wa vifaa ambapo kwa sasa Serikali imeliwekea mkazo suala
hilo ili kuhakikisha kina mama hao wanajifungua salama.
Post a Comment