Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

RAIS MSTAAFU JK AENDELEA NA JUHUDI ZA USULUHISHI WA MGOGORO WA LIBYA



Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa
Afrika katika Mgogoro wa Libya ameendelea na juhudi zake za usuluhishi
wa mgogoro wa Libya kwa kushiriki katika Kikao cha 11 cha Mawaziri wa
Nchi Jirani na Libya kilichofanyika jijini Algiers, Algeria tarehe 8
Mei, 2017.

Katika Kikao hicho, Rais Mstaafu amepongeza juhudi  zinazoendelea za kupatanisha pande zinazogombana nchini Libya na  mafanikio yanayopatikana ikiwemo kuimarika kwa hali ya usalama, kudhibitiwa kwa vitendo vya kigaidi, kuongezeka kwa shughuli za
uzalishaji wa mafuta na kufufuliwa kwa mawasiliano kati ya pande zinazohasimiana.


 

 Ameunga mkono jitihada zinazochukuliwa na nchi za Algeria, Misri, Tunisia na UAE katika kuhimiza mazungumzo ya Amani. Amesisitiza umuhimu wa pande mbili za mgogoro kuheshimu Makubaliano ya Amani ya Libya (Libya Political Agreement) na kutekeleza vipengele vyake bila ajizi.

Akiwa jijini Algiers, Rais Mstaafu amefanya pia mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo anayemuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kuhusu Libya Mhe Jean-Claude Gakossona Balozi Martin Kobler, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mgogoro wa Libya (UNSMIL).

Rais Mstaafu anatarajiwa kumalizia ziara yake nchini Libya kukutana na viongozi wakuu wa pande zinazotofautiana nchini humo.
 
Rais Mstaaafu Dkt Jakaya Kikwete akifuatilia Mkutano wa Nchi Majirani wa Libya Ameunga mkono jitihada zinazochukuliwa na nchi za Algeria, Misri, Tunisia na UAE katika kuhimiza mazungumzo ya Amani. Amesisitiza umuhimu wa pande mbili za mgogoro kuheshimu Makubaliano ya Amani ya Libya (Libya Political Agreement) na kutekeleza vipengele vyake bila ajizi.

Akiwa jijini Algiers, Rais Mstaafu amefanya pia mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo anayemuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kuhusu Libya Mhe Jean-Claude Gakossona Balozi Martin Kobler, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mgogoro wa Libya (UNSMIL).


Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwakilishi wa  Umoja wa Mataifa katika Mgogoro wa Libya Balozi Martin Kobler jijini Algiers.



 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akitoa msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu Mgogoro wa Libya .
Rais Mstaafu katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo na Mwenyekiti wa AU Mhe. Jean-Claude Gakosso. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi ya Uwakilishi wa AU kwa Libya Bi. Wahida Ayari
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget