Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.


0151-Mhe.Mwinyi
Na Husna Saidi & Nuru Juma
Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa inampango wakuunda kikosi kazi cha kupitia changamoto zinazowakabili Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Sita kutojiunga na mafunzo yaJeshi kama sheria ya Jeshi la kujengaTaifa inavyotaka.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Hussein Mwinyi alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na George Huruma Mkuchika Mbunge wa jimbo la Newala Mjini.

Dkt. Mwinyi alisema kuwa Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 1964 imeweka ulazima wa vijana wa Tanzania wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria, hatahivyo mwaka 1994 Serikali iliyasitisha kwa muda mafunzo hayo na kuyarejesha tena mwaka 2013 na yanaendelea hadi sasa.
“Takwimu zilizopo zinaonyesha kupungua kwa idadi ya vijana wanaojiunga na mafunzo hayo muhimu ya jeshi la kujenga Taifa hali hii imesababishwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugongana kwa tarehe za kuanza mafunzo ya vijana kwa mujibu wa sheria na kufunguliwa kwa vyuo mbalimbali hapa nchini ambapo mihula ya mafunzo huanza”, alisema Dkt. Mwinyi.
Aidha alisema hali hiyo imewafanya vijana wengi walioteuliwa kujiunga na vyuo kukosa nafasi ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwamujibu wa sheria na changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu, rasilimali watu na pamoja na fedha, hatahivyo Serikali inaendelea na juhudi za kupata suluhu ya changamoto hizo.
Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa mwaka 2014 vijana waliohitimu kidato cha sita walikuwa 41,968 na kati yao waliojiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa walikuwa 31,692 ambao ni sawa na asilimia 75.5.
Aidha mwaka 2015 kulikuwa na wahitimu 40,753 na waliojiunga ni 19,990 sawa na asilimia 48.8 huku mwaka 2016 wahitimu kidato cha sita walikuwa 63,623 waliojiunga na Jeshi ni 14,747 sawa na asilimia 23.2.
Zoezi la kuwachagua vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa halina vigezo maalum kwani kila kijana aliyemaliza kidato cha sita anasifa ya kujiunga na mafunzo hayo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget