Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI


PMO_6318
Na Nuru Juma & Husna Saidi
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaendelea na kutekeleza  miradi mbalimbali ya maji Mijini na Vijijini ili kuhakikisha Taifa linaondokana na kero itokanayo na maji.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge alipokuwa akijibu swali la Mhe, Leah Jeremiah Komanya Mbunge wa viti Maalum.

Mhandisi Lwenge alisema katika kuhakikisha miradi hiyo inanufaisha jamii kama ilivyokusudiwa Wizara yake imeandaa na inatekeleza uundaji, usajili wa vyombo vya watumiaji maji (COWSOs) na kuzijengea uwezo kwaajili ya uendeshaji na usimamizi.
“Pamoja na utekelezaji huo kumekuwa na changamoto mbalimbali katika miradi hiyo ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya maji, wizi wa vifaa vya maji pamoja na watumiaji maji kutolipa huduma hiyo zikiwemo taasisi za Serikali hali hiyo imepelekea mamlaka nyingi kushindwa kugharamia matengenezo ya miundombinu ya maji” alisema Mhandisi Lwenge.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na wizi wa maji pamoja na uchakavu wa miundombinu Wizara inaendelea kurekebisha Sheria za maji ili ziweze kutoa adhabu kali kwa wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji.
Aidha alisema kuwa katika kuhakikisha mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira zinatoa huduma endelevu mamlaka hizo zinasimamiwa na bodi ambazo zinajumuisha wadau mbalimbali.
Kwa upande mwingine alisema mamlaka za maji  safi na usafi wa mazingira mijini zinaendelea kukarabati miundombinu ya maji iliyochakaa, kufunga dira za maji kwa wateja wote ili kubaini matumizi yao halisi na kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya maji.
Aidha Wizara imeanza kuchukua hatua za kutumia nishati ya jua kwenye mitambo ya maji hususani vijijini kwaajili ya kupunguza gharama za uendeshaji.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget