Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

TAARIFA ZA CHAMA KWA WIKI CHACHE ZILIZOPITA MPAKA 14 MAY, 2017

Image result for CHAMA CHA WANANCHI CUFTHE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
 
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
 
Imetolewa leo Tarehe 15/5/2017
 
TAARIFA ZA CHAMA KWA WIKI CHACHE ZILIZOPITA MPAKA 14 MAY, 2017
 
Hii ni wiki ya saba (15) sasa kukuletea mukhtasari wa taarifa muhimu za Chama juu ya masuala mbalimbali kwa lengo la kuwajulisha wanachama, viongozi na watanzania kwa ujumla yanayoendelea ndani ya CUF na kuwekana sawia kwa kuwapa hali taarifa (Updates) na aidha kusahihisha taarifa za upotoshwaji, hujuma na au propaganda chafu dhidi ya Chama.
 
KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA WIKI HII INAWAJULISHA TAARIFA ZIFUATAZO:-
 
1.      (A) KATIBU MKUU, MAALIM SEIF KUWATEMBELEA WAZEE WAASISI WA    
       CUF, KUWAJULIA HALI WAGONJWA NA KUWAFARIJI WAFIWA   
       KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM:
Katibu Mkuu,Maalim Seif Sharif Hamad, amewatembelea na kuwajulia hali wazee waasisi wa CUF, wagonjwa na kuwafariji wafiwa mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam. Maalim Seif amepata mapokezi makubwa na ya heshima kila alipofika. Wananchi na Wanachama wengi wamekuwa na hamu kubwa ya kufikiwa na ziara hiyo na kila mmoja kutaka afike katika Kata na au Tawi lake la Chama. katika ziara hiyo Maalim Seif aliambatana na Wakurugenzi wa Chama Taifa, Wajumbe wa Baraza Kuu. Wabunge –CUF na Manaibu Meya wa Dar es Salaam. Katibu Mkuu ataanza ziara ya ukaguzi wa Uhai na Shughuli mbalimbali za Chama katika Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.   
 
(B)KATIBU MKUU KUMTEMBELEA ASKOFU GWAJIMA:
Tarehe 10/5/2017 Maalim Seif alimtembelea Askofu Josephat Gwajima Ofisini kwake Ubungo- Dar es Salaam kumjulia hali na kubadilishana nae mawazo juu ya masuala mbalimbali nchini. Baadae walipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo walieleza kuwa wao ni marafiki na wamekutana kubadilishana mawazo.  
 
2.      MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI TAIFA MHE.JULIUS MTATIRO AFANYA ZIARA TANGA MJINI:
Mheshimiwa Julius Mtatiro amefanya ziara ya kichama na kufanya kikao na Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Tanga. Ziara hiyo ilisitishwa na Jeshi la Polisi kwa kisingizio eti cha  uvunjifu wa amani kutokana na sababu za kiintelijensia. Pamoja na awali Jeshi hilo kupokea taarifa ya ziara hiyo na kuruhusu kufanyika. Ghafla siku ya ziara hiyo OCD-Tanga aliandika barua ya kusitisha ziara hiyo, pamoja na kufanya nae mazungumzo na kujenga hoja ambazo alishindwa kuzijibu aliendelea na msimamo huo kwa maelekezo kuwa amepata maagizo kutoka ngazi za juu. Awali Jeshi hilo na uongozi wa Mkoa lilitaka kuwatumia kuwagawa madiwani wa CUF na viongozi wa CUF ionekane kuwa kuna tofauti miongoni mwao ili wapate sababu lakini hawakuweza kwani viongozi wote wa Tanga walikuwa kitu kimoja Kumpokea Mwenyekiti wao Taifa Mhe. Julius Mtatiro.
 
 
3.     TAARIFA YA KESI ZA CHAMA NAHATUA ZA KISHERIA JUU YA  UVAMIZI WA WAFUASI WA LIPUMBA VINA HOTEL, MABIBO DAR ES SALAAM:-
 
a)      Shauri la msingi namba 23/2016 lililopo kwa Jaji Kihiyo dhidi ya Msajili Jaji Francis Mutungi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Lipumba na wenzake limepangwa kutajwa tena Tarehe 18/5/2017.
b)     Mashauri yote yanayohusiana na wizi wa fedha za Ruzuku yamepangwa kusikilizwa Tarehe 6/6/2017  Kesi zote kwa ujumla zinaendelea na kusimamiwa vizuri na mawakili wetu.
c)      Suala la Uvamizi wa wafuasi wa Lipumba Vina Hotel na kuwajeruhi waandishi wa Habari na viongozi wa CUF katika Mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Juma Mkumbi bado lipo mikononi mwa Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Mhe Simon Sirro. Mpaka sasa watuhumiwa hawajafikishwa Mahakamani.
 
4.     KAZI ZA MANAIBU MEYA WA DAR ES SALAAM MHE. MUSA KAFANA (JIJI), MHE. OMARI KUMBILAMOTO NA MHE. RAMADHANI KWANGAYA:
Naibu Meya wa Jiji na Manispaa ya Ilala na Ubungo, Dar es Salaam wameendelea kuwatumikia wananchi wao na kukitumikia Chama katika maeneo yao. Mhe. Kumbilamoto ametoa Mashine ya Kuoshea magari kwa vijana wake wa Vingunguti, Jezi seti tatu, na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo kiongozi wa wabunge wa CUF Bi. Riziki Shahali Ngw’ali, Mhe. Kuchauka na wadau wengine.  Manaibu Meya wamewatembelea waathirika wa Mafuriko katika maeneo mbalimbali ya wilaya zao na Mhe Kwangaya amesimamia mradi wa uchimbaji wa visima vya maji kwa wananchi wake wa wilaya ya Ubungo.
 
5.     CHAMA KIMETUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA KUTOA POLE KWA MSIBA WA WANAFUNZI 32 NA WALIMU ULIOTOKEA ARUSHA, NA KUWAPA POLE WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI IKIWEMO TANGA, LUSHOTO, PEMBA NA UNGUJA: Mhe Saumu Sakala (MB) alikiwakilisha Chama katika msiba wa wanafunzi Jijini Arusha.  Aidha, Viongozi wa kambi ya CUF bungeni wameratibu safari za wabunge kuwafikia wananchi katika majimbo yao kwa awamu ili kuwafariji waathirika wa mafuriko hayo: waliokwenda Majimboni katika awamu hii ni Mhe. Twahir Awesu Mohamed (Mkoani), Mhe. Khalifa Mohamed Issa (Mtambwe), Hamad Salim Maalim (Kojani), Mhe. Dr, Suleiman Ali Yusuf (Mgogoni), Mhe. Khatib Said Hajji (Konde), Mhe. Haji Khatib Kai (Micheweni), Mhe. Mbarouk Salim Ali (Wete), Mhe. Abdallah Ally Mtolea (Temeke), na Mhe. Yussuf Kaiza (Chakechake).
 
6.      MWENENDO WA JESHI LA POILISI, UDHAIFU NA WOGA WA SERIKALI YA CCM YA AWAMU YA TANO KWA VYAMA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZA KISIASA:
Jeshi la Polisi limekuwa likitumika vibaya kuhujumu shughuli za kisiasa zilizoanishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Vyama vya Siasa. Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Magufuli imekuwa na UDHAIFU NA WOGA MKUBWA WA KUKOSOLEWA, KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA NA KUFANYA VITENDO VYA KUKANDAMIZA DEMOKRASIA. Mbali na kuzungumza mara kadhaa juu ya suala hili na viongozi wa Jeshi la Polisi inaonekana pamoja na baadhi yao kuwa na nia njema na kuchoshwa na mashinikizo yanayotokana na Viongozi wa Kisiasa wa Serikali ya CCM bado vitendo hivyo vya kuihujumu CUF na viongozi wake vimekuwa vikiendelea kwa kushirikiana na vibaraka wao ndani ya CUF. Ni Aibu kwa Serikali inayojigamba kuwa imeshinda Uchaguzi kwa ridhaa ya wananchi kuogopa vyama kufanya shughuli zake, kuogopa kukosolewa na kuzuia shughuli halali za kisiasa za vyama. CUF inaendelea kulishughulikia suala hili na kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa kudumu unapatikana ili kuepusha machafuko makubwa siku za usoni. Inashangaza kuona kuwa eti jeshi la Polisi matahalani linapewa taarifa za kusudio la uvunjifu wa amani kwa barua na watu wanaofahamika! Linaacha ‘kudeal’ na waliotoa taarifa hiyo wanaokusudia kufanya vurugu, badala yake linajiandaa kutumia NGUVU KUBWA na kuandaa vikosi vya majeshi kuzuia shughuli za Chama za kikao cha ndani tu na wakati mwingine kiako hicho hakizidi watu 40. Tuna kila sababu Vyama vya Upinzani nchini kufikiria njia mbadala za kukabiliana na kukomesha hali hii.
 
7.   USAFI OFISI KUU YA CHAMA BUGURUNI UPO PALEPALE:
 
Zoezi la kufanya usafi katika ofisi kuu ya chama buguruni haliepukiki kutoka na ofisi hiyo sasa kugeuzwa kichaka na kijiwe cha wahuni, kupanga na kuratibu utekaji na kushambulia wananchi, wanachama na viongozi wa CUF, uharibifu wa mali za chama, gari za Chama kutumika kwenda kuzikia majambazi, kufanyika kwa vikao haramu, kukaribisha na kuwaficha wahalifu mbalimbali na wengine wenye silaha za moto, Ofisi Kuu kugeuzwa Danguro na makaazi ya wahalifu na waliokosa sehemu za kulala, kutumika kuanzisha mradi wa mamalishe na kuonekana jungu la DONA likipikwa na kusababisha uchafuzi wa mazingira, vyoo vimeharibiwa na hakuna usafi unaofanyika. Kwa ufupi hakuna la maana linalofanyika kwa maslahi ya Chama cha CUF na Taifa kwa ujumla. Lazima usafi ufanyike ili kuirejeshea heshima Ofisi ya Chama. Mhe. Abdallah Mtolea (MB) kiongozi mratibu wa zoezi hilo anawataka wana-CUF wote kuendelea na kufanya maandalizi ya kutosha kutokana na makubaliano yetu na Viongozi husika kumalizika na hakuna hatua zilizochukuliwa. Wakati wowote kuanzia sasa Mtajulishwa ni namna ipi itumike kuondoa uchafu (Najisi) iliyojaa Ofisi Kuu, Buguruni.
 
 
HAKI SAWA KWA WOTE
 
----------------------------------------------
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA, CUF-TAIFA
 
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget