Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MV KAZI YAFANYIWA MAJARIBIO

unnamed
Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari.
A
 Magari yakiingia kwa mara ya kwanza kwenye kivuko kipya cha MV KAZI tayari kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika.

A 1
 Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
A 2
 Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
A 4
 Kivuko cha MV KAZI kikiondoka kwa mara ya kwanza kutokea Magogoni kuelekea Kigamboni kikiwa na abiria na magari. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio mara baada ya ujenzi wake kukamilika kabla ya kukabidhiwa  kwa TEMESA.
A 3
Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
A 5
 Abiria wakishuka kutoka katika kivuko cha MV KAZI mara baada ya kuwasili upande wa Kigamboni kwa majaribio, ujenzi wa kivuko hicho umekamilika na kinategemewa kuanza kutoa huduma hivi karibuni.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA) 
……………………….
ALFRED MGWENO
Kivuko cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari  kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza  kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo. Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. 
Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Miongoni mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.
Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget