Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

NAIBU WAZIRI NGONYANI AWATAKA MAKANDARASI BARABARA YA MAFINGA - IGAWA KUONGEZA KASI


ig1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipitia taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Mafinga –Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 Mkoani Iringa mara baada ya kukagu mradi huo kulia ni Meneja Mradi huo Richarad Guo akisisitiza jambo.
ig2
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga –Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 Richarad Guo alipokagua ujenzi huo Mkoani Iringa.
ig3
Muonekano wa barabara ya Mafinga –Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 ambapo tayari Kilomita 18 zimekamilika kwa kiwango cha lami, ujenzi huo unafanywa na kampuni ya China Civil Engenering Construction Corporation (CCECC).
ig4
Mafundi wanaojenga barabara ya Mafinga-Igawa  sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 Mkoani Iringa wakiendelea na ujenzi wa karavati kubwa katika eneo chepechepe maarufu Majinja wilayani Mufindi.
ig5
Muonekano wa Mtambo wa kusaga kokoto pamoja na shehena ya kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Mafinga –Igawa.

…………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amemtaka mkandarasi China Civil Engeneer Construction Cooporation (CCECC), anayejenga barabara ya Mafinga-Nyigo km 74.1 na (CRSG) anayejenga sehemu ya Nyigo –Igawa KM 63.8  kuongeza kasi ya ujenzi ili upanuzi na uimarishaji wa barabara hiyo ukamilike kwa wakati.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Eng. Ngonyani amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Iringa Eng. Daniel Kindole kuhakikisha upana wa barabara hiyo na ubora wake unakidhi malengo ya Serikali ili barabara hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kupunguza msongamano na ajali zinazoepukika.
“Barabara hii ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya TANZAM inaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi za Zambia na Malawi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi hivyo ni lazima isimamiwe kikamilifu ili idumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Eng. Ngonyani.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa Eng. Daniel Kindole amesema tayari kilomita 18 kati ya 74.1 katika sehemu ya kwanza ya Mafinga –Nyigo imeshawekwa  lami na Mkandarasi ameunda timu tatu ili kuharakisha ujenzi huo.
“Ujenzi wa barabara ya Mafinga -Igawa unahusisha mikoa mitatu ambapo Kilomita 74.1 ziko katika mkoa wa Iringa Mafinga-Nyigo, Kilomita 52 ziko katika mkoa wa Njombe Nyigo-Halali na Kilomita 12 ziko katika Mkoa wa Mbeya Halali-Igawa hivyo mimi pamoja na wenzangu tumejipanga kuhakikisha barabara hii inakamilika Novemba mwakani kama ilivyopangwa”, amesisitiza Eng. Kindole.
Naye Meneja Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo Sehemu ya Mafinga – Nyigo KM 74.1 Richard Guo amemhakikishia Naibu Waziri huyo kwamba kasi yao ya ujenzi ni nzuri na barabara hiyo imeimarishwa ili kukidhi mahitaji na itakamilika kwa wakati.
Zaidi ya shilingi bilioni 116 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara hiyo sehemu ya kwanza yaani Mafinga- Nyigo km 74.1 ambazo zinagharamiwa na Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget