Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Ujerumani kufunga biashara ya Korea Kaskazini

City Hostel Berlin
SERIKALI  ya Ujerumani inapanga kufunga biashara inayofaidi taifa la Korea Kaskazini katika jiji la Berlin.

Hatua hiyo, ya kufunga bweni kubwa ambalo linapatikana katika kipande kimocha cha ardhi na ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Berlin, inaambatana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambao umewekewa taifa hilo.

Lengo la vikwazo hivyo ni kuzuia taifa hilo la kikomunisti kustawisha silaha zake za nyuklia ambapo bweni hilo kwa jina City Hostel Berlin huendeshwa na kampuni ya biashara za hoteli ya Uturuki ambayo hulipa zaidi ya €38,000 (£32,000; $41,000) kama kodi kwa Korea Kaskazini.

Ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Berlin pia hujipatia mapato kwa kukodisha ukumbi ulio katika eneo palipojengwa bweni hilo.
Korea Kaskazini imetekeleza majaribio kadha ya silaha za nyuklia na pia majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Hilo limeibua wasiwasi kwamba huenda karibuni ikawa na makombora ya nyuklia yanayoweza kufikia Japan au Marekani.

City Hostel Berlin ilijengwa zamani katika Ujerumani Mashariki ambayo ilikuwa ya Kikomunisti kabla ya kuungana tena kwa taifa hilo na Ujerumani Magharibi na kuwa Ujerumani ya sasa.

Bweni hilo lilitumiwa kama makazi ya wafanyakazi wa ubalozi.
Ni maarufu sana kwa watu wanaosafiri Berlin kutokana na gharama yake nafuu.
City Hostel BerlinHaki miliki ya picha EPA picha                                    Bweni hilo huwa nafuu kwa wageni                
Inakadiriwa kwamba mgeni anaweza kukaa katika bweni lenye vitanda vinane kwa kulipa €9.50 kila siku.

Azimio 2321 la Umoja wa Mataifa ambalo liliidhinishwakwa kauli moja Novemba mwaka jana lilikaza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanya jaribio la silaha za nyuklia tarehe 9 Septemba.

Azimio hilo huyataka mataifa yote wanachama kuizuia DPRK [Korea Kaskazini] kutumia nyumba ama ardhi inayomiliki au kukodi katika mataifa husika kwa matumizi mengine ila shughuli za kibalozi".

Markus Ederer, katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, amesema "ni sharti tuongeze shinikizo ili kuhakikisha Korea Kaskazini inarejea kwenye meza ya mazungumzo."
City Hostel BerlinHaki miliki ya picha Reuters
Image caption Bweni hilo linapatikana katika kipande kimoja cha ardhi na ubalozi wa Korea Kaskazini
Vikwazo hivyo vya Umoja wa mataifa vinafaa kutekelezwa kikamilifu, alisema, "kwa hivyo ni muhimu sana tuzime shughuli ambazo zinaweza kutumiwa kupata pesa za kufadhili mpango wa nyuklia (wa Korea Kaskazini)".

Chanzo BBC News.

Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget