DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA VITABU
Mwagala
Wananafunzi wa Shule za
Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili
waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na
wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho,
wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo.
Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza
wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi
Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo
Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation
kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa
mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe
taaluma hiyo.
Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru
akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu
kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau
wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.
Aidha Mama Jaqueline Mengi
amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo
la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za
msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu.
Shule ya Msingi Makumbusho
inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika
kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na
Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika
shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam.Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini kwake
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. Katikati
ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya
Kinondoni katika uzinduzi huo.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akibadilishana
mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha Afisa Elimu wa
Wilaya ya Kinondoni.Picha
juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama
Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho
kabla ya uzinduzi huo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi wa Dr.
Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la uzinduzi
wa maktaba hiyo.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa
Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni
wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma moja ya
vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho
waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi na Afisa Taaluma
Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni kwa
pamoja wakizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim (wa pili kulia).Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Makumbusho wakisoma vitabu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Dr. Ntuyabaliwe Foundation.Picha
juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama
Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule
wakikagua vitabu katika maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao.Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule.Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo (katikati) akionyesha
waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) muonekano wa
awali kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation.
Kushoto ni Mama Mengi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Shule, Haji
Shabani Kibwana.Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba
na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa
shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.
KAWAIDA
Wananafunzi wa Shule za Msingi
jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili
waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na
wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho,
wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo.
Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Post a Comment