Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

IGP Sirro afanya mabadiliko, SACP Kaganda kuhamia makao makuu ya Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Suzan Salome Kaganda, pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Murilo Jumanne Murilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Leo na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP Barnabus Mwakalukwa kwa vyombo vya habari, inaeleza kuwa SACP Kaganda amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi, na kwamba nafasi yake ya awali imechukuliwa na ACP Murilo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga. 
Pia ripoti hiyo inaeleza kuwa, nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Haule ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mara.
 
Aidha, taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa, uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya jeshi hilo katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget