Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MAKAMU WA RAIS AWA MLEZI WA GIRL GUIDES TANZANIA

liu1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Sania Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kukabidhiwa ulezi wa chama cha Girl Guides Tanzania kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
liu3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Sania Suluhu Hassan akikabidhiwa bendera kama ishara ya kukubali ulezi wa chama cha Girl Guides Tanzania kutoka kwa Mlezi aliyemaliza muda wake Mama Salama Kikwete ambaye amekuwa mlezi wa taasisi hiyo hapa nchini kwa miaka 12, hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyikakwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
liu4
Baadhi ya wanafunzi wakiimba shairi.
………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi nchini kuwalea vijana wao katika maadili mema ili waje kuwa viongozi au raia wema ambao watakaoliletea taifa tija na sifa ya uongozi bora ndani na nje ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo hayo katika hafla ya kukabidhiwa kuwa mlezi wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kutoka kwa mlezi anayemaliza muda wake Mama Salma Kikwete katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ili kazi ya kujenga maadili mema iweze kufanyika vizuri nchini ni muhimu kwa wananchi wote kuunga mkono jitihada zinafanywa na Serikali kwa sasa za kupambana na watu wanaovuruga maadili ya Kitanzania ili tabia hiyo iweze kukomeshwa haraka.
Amesema kuwa Serikali imejipanga ili kuhakikisha rasilimali zinazopatikana nchini zinanufaisha wananchi wote wakiwemo vijana wa kike na wa kiume.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amekipongeza Chama cha Tanzania Girl Guides Association kwa jitihada zake za kueneza misingi na stadi za kuishi kwa uadilifu,uzalendo kwani kufanya hivyo wanajenga taifa lenye watu waadilifu.
Makamu wa Rais pia ameuhakikishia uongozi wa chama hicho kuwa atakuwa nao bega kwa bega katika kuhakikisha chama hicho kinajiendesha kwa faida bila kutegemea wafadhili ambao wanazidi kupungua kila uchao.
“Niwaombeni mbuni mpya za kujiongezea kipato ili kuwaongezee uwezo wa kujiendesha mbinu hizo ni kama kutumia ardhi mliyonayo kwa kukopa benki au kuingia ubia na makampuni yaliyo tayari kushirikiana nanyi ili muweze kujenga majengo yenu ambayo mtaweza kupangisha na kupata kodi ambazo mtaweza kujiendesha, kujiongezea kipato na kuendesha chama kwa tija na ufanisi zaidi”. Amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake, Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides Association aliyemaliza muda wake Mama Salma Kikwete amesema katika kipindi cha uongozi wake chama hicho kimeweza kuongeza idadi ya wanachama kutoka 97,000/=mwaka 2015 hadi zaidi ya wanachama 100,000 kwa sasa na jitihada hizo bado zinaendelea.
Amesema anaimani kuwa chini ya Uongozi wa Mlezi mpya Mhe Samia Suluhu Hassan Chama hicho kitafanya kazi vizuri zaidi katika kuwalea vijana wa kike katika maadili mema ili waweze kujiepusha na vitendo vibaya katika jamii ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam
12-Julai-2017.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget