Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Jiji la Dar es Salaam lapata hati safi, Meya Mwita atoa iri ya hati hiyo



NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam imepata hati safi kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani la halmashauri ya jiji iliyokuwa na ajenda moja ya kuwasilisha taarifa ya CAG, Mstahiki Meya Isaya Mwita alisema kuwa hati hiyo imetokana na kuwepo kwa usimamizi mzuri wa matumuzi ya fedha.

Alifafanua kuwa kwa kiasi kikubwa tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ,jiji la Dar es Salaam lilisimamia na kupunguza matumizi ya fedha ambayo hayakuwa ya lazima jambo ambalo limeleta heshima kubwa katika halmashauri hiyo.

Aliongeza kuwa mbali na hiyo, lakini pia kwa kiasi kikubwa mapato ya jiji yameongezeka kutokana na kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya jiji hilo.

Alifafanua kuwa hati hiyo inaleta heshma kubwa ndani ya jiji na kwamba imetoa nafasi kwa watendaji ndani ya halmashauri kufanya kazi kwa umahiri zaidi ili kuweza kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi.

Alisema taarifa ya CAG imeeleza wazi kuwa hali ya utekelezaji  ndani ya jiji ni ya kuridhisha kutokana na usimamizi wa kutosha ,kufuatilia mambo na hivyo kuweza kuyafanyia kazi mapendekezo ya ukaguzi wa miaka ya nyuma yaliyosalia.

 Baada ya kupata hati hii, sasa niwakati mwingine jiji kuendelea kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zao, ukiangalia tumepewa dhamana kubwa ya kuwatumikia ,hivyo kama Meya mwenye jiji sina budi kuwatumikia wananchi kama inavyotakiwa” alisema Meya Mwita.

Aidha Meya Mwita alitoa wito kwa halmashauri zilizopo ndani ya jiji la Dar es Salaam kuwatumikia wananchi ikiwemo kutatua kero zinazo wakabili.

Wakati huo huo ,Meya Mwita alisema kuwa jiji limetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kununua maeneo ya makaburi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya maeneo ya kuzikia watu.
Alisema kwasasa hali imekuwa mbaya kwenye maeneo ya jiji na kwamba pesa hizo zitatumika kununua maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kuzikia watu wanapopoteza maisha.

 “ Jambo hili litaanza kufanyika mwaka huu, kila halmashauri itapatiwa eneo kwa ajili ya kuzikia watu, yapo maeneo ambayo tumepanga kuyanunua, ukiangalia jiji letu lina watu wengi sana, kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanavyozidi kuongezeka.

Leo hii imefikia hatua mtu ana zikwa juu ya mtu mwingine, jambo hili sio zuri, hata wandishi wa habari leo nikiwaualiza akifa mtu hapa anazikwa wapi, hakuna sasa utekelezaji wa jambo hili utaanza kufanyika mwaka huu” alisema Meya
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwasikiliza wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji waliokuwa wakichangia taarifa iliyowasilishwa kwenye baraza hilo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Katika taarifa hiyo, jiji la Dar es Salaam lilipata hati safi.

Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmshauri ya jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji, aliyekaa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji Waziri Kombo


Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget