Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).

Uzinduzi huo  ulihudhuriwa na  kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo  la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue, Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

APRM ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi  wanachama kujitathmini kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao.

 “Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti  ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



Baadhi ya wageni mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Mkutano huo.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget