Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WAZIRI JAFFO AONYA WATAKAOKWAMISHA JITIHADA ZA GREEN VOICES KUPAMBANA NA MAZINGIRA



Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) akisikiliza maelezo kutoka kwa mama Abia Magembe kuhusu bidhaa zinazotokana na zao la muhogo. Kushoto kabisa ni Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia Cebada na kulia ni Mratibu wa mradi huo nchini Tanzania, Secelela Balisidya.


NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, amesema halmashauri zinawajibu wa kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.


Kutokana na hali hiyo, ameonya mtu yeyote asikwamishe jitihada zinazofanywa na akinamama washiriki wa mradi wa Green Voices Tanzania huku akiahidi kuwa serikali iko nao bega kwa bega. Alisema kwamba, endapo kuna mtu katika idara zilizo chini ya wizara yake atakwamisha jitihada zao, basi akinamama hao wawasiliane naye moja kwa moja.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Green Voices nchini Tanzania uliofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Jaffo alisema kwamba, wizara yake ndiyo yenye jukumu kubwa la kuwawekea mazingira mazuri akinamama hao kutekeleza miradi yao chini ya halmashauri husika, hivyo akawaahidi kuwapatia ushirikiano wa kutosha kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu na suala la mazingira linapewa kipaumbele.


Mradi wa Green Voices unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Kigoma, Mwanza na Kilimanjaro, kukiwa na miradi 10 ikiwemo ya kilimo cha mihogo, kilimo cha matunda, uyoga, ufugaji wa nyuki, ukaushaji wa mbogamboga na utengenezaji wa majiko rafiki wa mazingira.

Bidhaa za mbogamboga zilizokaushwa kutoka Morogoro.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget