Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mhe. Makame Mbarawa afanya ziara JNIA

DSC_9236
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango (kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba na Katibu Mkuu  sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye mkoba mweusi) leo walipokutana kwenye Jengo la Watu Mashuhuri la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
DSC_9258
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), Bw. Joseph Nyahende (wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi wa namna abiria wenye viza  wanavyohudumiwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani). Pembeni ya Waziri ni Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho na nyuma mwenye suti nyeusi ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Salim Msangi
DSC_9311
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika kulipia viza kwa Mhe. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho.
ziara2Afisa Forodha Msaidizi, Bw. Hezron Giso (kulia), akielezea shughuli anazozifanya ndani ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani), wakati wa ziara ya Waziri iliyofanyika leo.
ziara3Afisa wa Benki ya NMB, Bi. Leah Rutayungurwa  (aliyendani ya dirisha) leo akimmsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa aliyetaka kujua muda anaohudumiwa abiria mmoja wakati akilipia viza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA).
ziara4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo akiwa katika mfumo wa kupokelea mizigo kwa abiria wanaowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali. Mwenye kizibao ni Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Bw. Joseph Nyahende.
ziara5Katibu Mkuu wa chama cha madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Simon Mwampashi (kulia), akitoa maoni mbalimbali kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo alipofanya ziara JNIA.
ziara6Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), mwenye kizibao akielezea jambo katika meza ya ukaguzi wa tiketi za abiria wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget