Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni mkombozi Afrika Mashariki

KC1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akipeana mkono na Kiongozi wa Msafara wa baadhi ya Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam.
KC2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akielezea jambo wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Bunge la Uganda waliotembelea Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wametembelea Taasisi hiyo ili kujionea namna inavyofanya majukumu yake.
KC3
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akizungumza jambo mbele ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (katikati).
KC4
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakifuatilia Maelezo kuhusu namna Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inavyofanya kazi wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
KC5
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya kuingia Wodi ya Watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam.
KC6
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote: Frank Shija – MAELEZO
………………………………………………………….
Na.Agness Moshi-MAELEZO
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha na ilivyokua hapo awali.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa  jimbo la Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili kuona na kujifunza  jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya kwa wananchi wake .
Bi.Cecilia  amesema  taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa  nchini India au Afrika Kusini  kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake watatibiwa Tanzania au nchini kwao.
“Tunahitaji kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya moyo“ Alisema Bi.Cecilia.
Bi Cecilia amesema  kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii  tangu kuanzishwa kwake  serikali ya Uganda imekubali  kuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.
“Hatukujua kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza Bi.Cecilia .
Naye Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utafiti wa Bunge la Uganda Mhe. Jonathan Enamu  amesema kuwa amejifunza mengi kwenye ziara hii na ameona ni jinsi gani gharama za matibabu zimepungua kwa wagonjwa wa moyo. “Nimejifunza mengi, ikiwemo jinsi ya kupunguza  gharama za matibabu na namna bima za afya zinavyoweza kutumika katika matibabu“ alisema Bw. Enamu.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi  amesema kuwa , wanatoa huduma kwa watu wote kuanzia daraja la chini  na watu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda,comoro,Yemen na Kenya.
 Prof.Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kutumia shilingi bilioni 1.65 badala ya shilingi bilioni 4.72 ambayo ni sawa na kupunguza takribani asilimia 65 ya gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini kama wangewapeleka India kwa matibabu
Prof. Janabi alifafanua kuwa kwa mgonjwa mmoja wa maradhi ya moyo anatibiwa kwa shilingi milioni 35-40 tofauti na nchini India ambapo mgonjwa mmoja anatumia shilingi milioni 120.
Aidha Profesa Janabi ameishukuru Serikali kwa kuipa ushirikiano taasisi hiyo kwani kwa mwaka huu wa fedha Taasisi imepokea asilimia 100 ya bajeti itakayosaidia kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha kuridhisha.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na  Mbunge wa ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu (MB) amesema  kuwa wamewapeleka  wageni hao kwenye taasisi ya moyo ili waweze kujifunza na kuona ni jinsi gani Tanzania imefanikiwa kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa moyo
“wameona namna sisi Tanzania tulivyopunguza gharama kutoka kuwapeleka watu 300 kwa mwaka nje kwa matibabu ya moyo mpaka sasa watu wanne tu, ambao tunawapeleka si kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu ya vifaa havijakidhi “ alisema Mhe.Zungu.
Taasisi ya  Moyo Jakaya Kikwete ilianzishwa rasmi mwaka 2014 inashughulika na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa moyo, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari,ufamasia na uuguzi. Pia taasisi hii inashirikiana na nchi nyingine duniani kwa kubadilishana maarifa,uzoefu na kufanya mafunzo mbalimbali.                               
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget