Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI LAENDELEA KUFANYIKA NCHINI


Na: Veronica Kazimoto



ZOEZI la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya

Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea nchi nzima

ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.




Akizungumzia zoezi hilo, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia

Meku wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema mpaka sasa mikoa kumi na

tatu (13) imekamilisha zoezi hilo ambapo ni sawa na silimia 50.


“Zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya

Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea vizuri na mpaka

sasa wadadisi wamekamilisha kuorodhesha kaya katika mikoa 13,”

amesema Sylvia Meku.


Ameitaja mikoa iliyokamilisha zoezi la uorodheshaji wa kaya kuwa ni

pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Iringa, Njombe na Morogoro.

Mikoa mingine ni Mwanza, Tabora, Katavi, Mbeya, Mara, Kagera na Lindi.

Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya linafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara na

linatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.





Utafiti kama huu mara ya mwisho ulifanyika Mwaka 2011/12 ambao

ulionesha kuwa asilimia 28.2 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa

Umaskini wa mahitaji ya Msingi.




Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka

2017/18 unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na

Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa

lengo la kupata viashiria vya kupima hali ya umaskini nchini.


Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa

za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato

na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18

linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia

kufanyika hivi karibuni.


Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa

za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato

na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18

linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia

kufanyika hivi karibuni.


Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwaoneyesha

wasimamizi namna alivyojaza taarifa za kaya wakati wa zoezi la

kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya

Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini

ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA).
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget