Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

TAHMEF yatoa huduma bure ya upimaji wa saratani ya shingo la kizazi wilayani Kondoa

Taasisi ya TAHMEF (Tanzania Health and Medical Education Foundation) limetoa huduma bure kwa wananchi wa wilaya ya Kondoa, Dodoma kupima saratani ya shingo la kizazi.
Zoezi hilo liliendeshwa kwa Muda wa siku mbili (8-9 Julai 2017) zaidi ya wanawake 500 Wilayani kondoa walijiandikisha na kupata huduma bure ya elimu na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Pamoja na kutoa huduma hiyo pia TAHMEF inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio na ajira rasmi na kuendelezwa harakati za kumfikia kila mtanzania kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watanzania juu ya changamoto mbalimbali za afya na jinsi ya kukabili changamoto hizo mapema.
TAHMEF ni shirika lisilo la kiserikali (NGO), lililozinduliwa rasmi tarehe 8 Julai 2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Wanawake wakazi wa Kondoa, Dodoma wakisubiri kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget