Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA NYUMBA ZA HALMASHAURI YA MOMBA



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwanachuo wa Chuo cha DIT, Grolia Shoo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba zinazojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba katika eneo la Chitete wialyani Momba Julai 21, 2017. Gloria anafanya kazi kwa muda akijifunza katika shirika hilo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC, Blandina Nyoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika eneo la Chitete akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. Wapili kulia ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalojenga nyumba hizo, Blandina Nyoni. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA wa kata ya Kangwa wilayani Songwe ,Keneth Nzowa ambaye pamoja na wenzake walitangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.

Wananchi wa Songwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadahara katika uwanja wa michezo wa Songwe Julai 20, 2017.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Chief Mwibongo wa Ivungu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget