Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Ujenzi wa Daraja la Kavuu lililopo mkoani Katavi wakamilika

Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na  Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.
“Serikali iliona kero kubwa wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.
Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari yatakayozidisha Tani 36.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua ujenzi wa Nyumba za Viongozi Mkoani humo na kuuagiza Wakala wa Majengo nchini (TBA), kuhakikisha  ujenzi wa nyumba hizo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.
“Serikali imeshatoa fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi, ujenzi huu ulisimama kwa takribani miezi minne kwa sasa hakuna sababu ya ujenzi kusuasua wakati fedha zipo, ninakuhakikishia Mkuu wa Wilaya nyumba hizi zitakamilika kwa wakati ili zianze kutumika,” alisisitiza Naibu Waziri Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Eng. Nyonyani amekagua ujenzi wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula.
Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget