Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

SHAKA:CCM HAIOKOTI VIONGOZI BARABARANI KAMA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI

 Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimsalimia Mama mwenye ulemavu na kumpatia
kiasi cha fedha alipokutananae wakati wa msafara wake kuelekea katika
uzinduzi wa Ofisi ya Tawi la Bugarika Kata ya pamba.
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya Tawi Bugarika wilayani nyamagana Mkoa wa Mwanza
 jiwe la msingi lililo wekwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wilayani nyamagana Mkoa wa Mwanza.
 Injinia
wa Barabara Ndg:Emilly Mbaga (kwanza kulia) akitolea ufafanuzi namna ya
kuandaa mawe kabla ya kutengeneza barabara ya mawe kwa Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (wa kwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Jimbo
la Nyamagana Ndg:Stanslaus Mabula wakati wa kushiriki ujenzi wa Barabara
ya mawe Wilayani Nyamagana kata ya pamba Bugando.
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (wa pili kulia)akishiriki Ujenzi wa barabara ya mawe kata ya Pamba Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza.
 Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) pamoja na Wanachama ,Viongozi mbali mbali wa
chama na jumuiya zake wakiwa na shamra shamra  alipowasili katika kikao
cha ndani pa
 Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM  Wilaya ya Nyamagana bi:Odilia Batimayo akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL.
  Baadhi ya mabango yakiwa na jumbe mbalimbali kwa ndg:Kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa ccm Ndg:Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg:Hussein Kim akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
Naibu Mstaiki Meya wa jiji la mwanza Mhe: Biku kotecha akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
 Mbunge wa jimbo la nyamagana Mhe:Stanslaus mabula  akisalimia
na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya mbunge jimbo la
nyamagana kwa vijana katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi
wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
ndg:Rooben Sixbert Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mwanza  akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) kuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
    Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  akuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Mathias Canal ,Nyamagana-Mwanza
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
umesema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake zote hakiokoti
wanachama barabani, uchochoroni, ama mtaani kama ilivyo katika vyama
vingine ambavyo sio CCM.
Umoja huo umesema kuwa kuokota Viongozi barabarani ni
kuzalilisha Chama na Jumuiya zake na kupoteza Misingi ya uwajibikaji na
utendaji ya kupata viongozi walioandaliwa kuanzia ngazi ya Shina, Tawi,
Mpaka Taifa.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 25, 2017 katika Ukumbi wa BELMOUNT
FIRMOUNT HOTEL uliopo Manispaa ya Nyamagana Wakati wa ziara ya siku moja
alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM)
pamoja na  wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM).
Shaka alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hufanya maandalizi
ya uchaguzi Mkuu pindi tu unapomalizika uchaguzi kwa kuwapata Madiwani,
Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza Kusimamia
na kufatilia utekelezaji wa ilani ya ushindi ya CCM.
Alisema kuwa anavionea huruma vyama vya upinzani kwani
havitaweza kuwa na mgombea Mwenye uwezo wa kushindana na Mwenyekiti wa
CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli kwani kazi kubwa anayoifanya nchini katika kipindi cha utendaji
wake kinaungwa mkono na Wananchi wote wakiwemo wale wa Chama vya
upinzani na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
“Vijana wenzangu napenda mtambue kuwa siku zote Kizuri
Chajiuza na kibaya chajitembeza, Hivyo Rais Magufuli ni KIZURI ambacho
kinajiuza chenyewe bila hata kutembezwa na mtu yeyote” Alisema Shaka
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kushinda
kwa haki, Amani na Demokrasia pasina vurugu, Ghubu, na visilani kama
inavyofanywa na vyama vingine visivyo CCM.
“Nataka niwakumbushe tu ndugu zangu wanachama wenzangu wa
Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa nchi yetu ya Tanzania haijawahi kuwa na
vyama vya upinzani Bali imewahi kuwa na vyama vya vurugu na kejeli dhidi
ya Serikali yao” 
“Ninazo taarifa kuwa kuna Kata moja wamepitishwa wahenga
kwenye uchaguzi wa Vijana sasa natoa maelekezo kwa Katibu wa UVCCM
Wilaya ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza kusimamia na kuwatoa haraka kwani
wakiwaacha mpaka wakaingia kwenye uchaguzi watakuwa wamekiuka taratibu
na Kanuni za Uchaguzi” Alisisitiza Shaka
Katika Ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo ameshiriki ujenzi
wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini na kuahidi kumalizia katika
upauaji jambo ambalo limemfanya pia Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe
Stanislaus Mabula kuchangia Bando tatu za bati ili kumuunga mkono Kaimu
Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka.
Aidha, Shaka ameshiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa
kiwango cha Mawe yenye urefu wa Kilomita moja kwani itatoa urahisi wa
Huduma za kijamii hususani kwa Wakati wa Kaya ya Mahina na Kata ya
Pamba.
Shaka amesisitiza mipaka ya kazi na kuwepo heshima kwa
kuchagua viongozi wenye sifa za kuchaguliwa huku akiwakumbusha Vijana
Kujiunga katika vikundi Mbalimbali ambavyo watavisajili na hatimaye
kuandika barua ya kuomba mikopo ambayo inatolewa na Serikali kwa riba
nafuu ya shilingi 50,000 kwa kila wanapokopa Milioni Moja.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget