Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

''Rais wa Nigeria kurudi nyumbani karibuni''

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kurudi hivi karibuni kwa mujibu wa makamu wa raisHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kurudi hivi karibuni kwa mujibu wa makamu wa rais
Rais wa  Buhari anaendelea kupona kwa haraka na atarudi nyumbani hivi karibuni ,kulingana na makamu wa rais ambaye ndiye kaimu rais Yemi Osinbajo.
Alitoa tangazo hilo katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatano asubuhi baada ya kumtembelea Buhari katika hospitali ya London ambapo anatibiwa ugonjwa usiojulikana.
Bwana Buhari amekuwa mjini London tangu mwezi Mei ambapo rais huyo mwenye umri wa miaka 74 alichaguliwa 2015, na kuwa rais wa kwanza kutoka kwa upinzani kushinda uchaguzi.
Ni mara yake ya pili kwenda katika likizo ya matibabu mjini London ,mara ya kwanza ikiwa mwezi Januari na alirudi nyumbani mnamo mwezi Machi.
Kutokuwepo kwake kumezua uvumi kuhusu iwapo ataendelea kuwa kiongozi wa taifa hilo.
Mapema wiki hii mkewe Aisha Buhari aliwashambulia maafisa wakuu wa chama tawala nchini humo wanaoshukiwa kupigania nyadhfa za urais na ile ya makamu wake huku mumewe akiwa mgonjwa.
Katika chapisho la mtandao wa facebook ,bi Buhari aliwaonya maafisi na mbwa mwitu kwamba watafukuzwa.
Hivi ndivyo mkewe Aisha Buhari aliandika katika Ujumbe wa facebookHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionHivi ndivyo mkewe Aisha Buhari aliandika katika Ujumbe wa facebook
Makamu wa rais amekuwa kaimu rais wakati wote ambao rais Buhari amekuwa nje ya taifa hilo lakini hakuna madai kwamba amekuwa akipanga njama dhidi ya rais Buhari kulingana na mwandishi wa BBC naziru Mikailu.
Matamshi ya bi Buhari yanajiri kufuatia chapisho la seneta Shehu Sani aliyeonya kwamba watu wanapanga njama za kuchukua urais.
CHANZO BBC NEWS
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget