Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

China: Nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini sio chaguo

Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Liu JieyiHaki miliki ya pichaUN WEB TV
Image captionBalozi wa China katika Umoja wa Mataifa Liu Jieyi
Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa amekiambia kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba suluhu ya nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini haifai kupewa kipao mbele, akijibu hatua ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu.
Liu Jieyi alirejelea wito wa China na Urusi kwa mazungumzo ya Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora iwapo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.
Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Nikki Haley alisema kuwa vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa Pyongyang kwa miaka kadhaa havitoshi.
Amesema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini ni ishara za kuzuka kwa mgogoro duniani.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget