Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Meya Mwita ashauri Halmashauri kuiunga mkono Serikali ya Viwanda

Displaying M5a.jpg
Displaying IMG_1426.JPGMstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Issaya Mwita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) walipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. 
Displaying M6.jpg
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata huduma ya kupima urefu mara baada ya kupima presha alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. 
Displaying IMG_1450.JPG

Displaying M1.jpg
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwatambulisha Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Issaya Mwita (kulia) na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta kwa ugeni kutoka Oman walipotembelea katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) jana
Displaying IMG_1483.JPG
Displaying IMG_1435.JPG
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

HALMASHAURI  zote Nchini zimetakiwa kutumia vyema fedha zinazotengwa kwa ajili ya kundi la vijana na wanawake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati na Viwanda.

Hayo yamebainishwa jijini hapa jana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta.

“Taasisi za kifedha zinao wajibu mkubwa katika kufikia adhima hii ya Serikali ya Viwanda, lakini sisi Serikali za mitaa pia , Halmashauri zinazo wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba zile asilimia tano za vijana na wanawake zinakuwa sehemu ya kuchochea ufanikishaji wa dhamira njema ya Serikali hii,” alisema Meya Mwita.

Aidha Meya  Mwita ametoa pongezi kwa uongozi wa Tantrade kutokana na jitihada zao za kuhakikisha wanasaidia ukuaji wa bidhaa za ndani hasa bidhaa za ngozi ambapo alisisitiza ni vyema wakaendelea kuweka mkazo katika eneo hilo kabla ya kuangalia maeneo mengine.

Mbali na pongezi hizo, Meya Mwita aliishauri Tantred kuwa katika kuendeleza dhamira ya maonyesho ya sabasaba ya Baba wataifa Hayati Julius Nyerere ,ni vema maonyesho hayo yakafanyika kwa kila mkoa, ili kutoa nafasi kwa wengine kuweza kushiriki kikamilifu na kujifunza mambo muhimu.
Alisema kuwa wapo watanzania ambao wangependa kushiriki na kuonyesha bidhaa zao lakini kutokana na changamoto za hapa na pale wakashindwa kufanikisha na hivyo kukosa haki yako ya kutoa elimu na kutangaza bidhaa zao.

“ Leo hii hapa ukiangalia washiriki waliopo kwenye maonyesho haya, ni wahapa, wengine kutoka nchi nyingine, nakwamba kama wapo wa mikoani sio wote, sasa vipi yule ambaye yupo Ifakara, Dumila, anabidhaa za kuonyesha lakini kashindwa kushiriki.

Mnaweza kumsaidiaje?, wakati wa maonyesho haya yalipoanzishwa mwalimu Nyerere alikuwa na dhamira ya kila mtanzania kutumia nafasi hii kuonyesha bidhaa zake, sasa hili nalo nashauri mliangalie ili muweze kutoa nafasi kwa kila mtanzania” alisisitiza Meya Mwita.

wa upande wake Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa Maonesho hayo ya Sabababa yamekuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wengi na hata kwa wananchi kuja kujifunza.

Aliongeza kuwa pamoja na wananchi kuja kujifunza lakini pia imekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mahusiano na wafanyabiashara wenzao kutoka nchi nyingine jambo ambalo katika biashara ni muhimu sana.

Nae, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin Ratageruka amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na soko la uhakika ndani na nchi ya nchi.

Ameongeza kuwa kwa kuanzia wamejikita zaidi katika bidhaa za ngozi ikiwa ni njia pia ya kuwainua wafugaji ambao mazao ya mifugo yao yanatumika katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi.

 “Serikali inatambua umuhimu wa kuthamini bidhaa za ndani, ndiyo sababu Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu zoezi ambalo jumla ya vijana 1000 walipatiwa mafunzo ya usindikaji na ushonaji wa ngozi, katika mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam tawi la Mwanza,” alisema Rutageruka.
Rutageruka ameongeza kuwa katika kuendeleza jitihada hizo Gereza la Karanga (Moshi) na Kampuni ya Woisso ya Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha viwanda kwa ajili ya kutengeneza sole ili kuachana na utaratibu wa kuagiza skutoka nje.

Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanafanyika huku adhima ya Serikali ya awamu ya tano ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda



Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget