
 Kaimu
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto), 
akikaribishwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa 
Wafanyakazi, (WCF), Bw. Sebera Fulgence, alipotembela banda hilo kwenye 
hema la Jakaya Kikwete viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba,
 barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya 
biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 4, 2017. Mhe Profesa 
Hamisi  alitumia kwa uchache dakika 15 akiwa na shauku ya kupata taarifa
 zaidi kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko huo. Mhe Profesa Hamisi 
alielezwa kuwa Mfuo huo umeundwa mahsusi kwa ajili ya kutoa fidia 
stahiki kwa Mfanyakazi aliyepata ugojnwa au kuumia mahala pa kazi. Hali 
kadhalika, alielezwa kuwa pamoja na kwamba Mfuko huo  ni wa Hifadhi ya 
Jamii, namna ya uchangiaji wake unatofautiana na Mifuko mingine, ambapo 
Mwajiri ndiye anawajibika kisheria kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi
 wakati Mifuko mingine, wachangiaji ni wote, mwajiri na mwajiriwa. 
Wakati hyuo huo, Waziri anayehusika na sekta ya Viwanda na Biashara, 
sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa wafanyakazi, naye alipata fursa ya 
kutembelea banda hilo ambapo kama ilivyokuwa kwa Kaimu Jaji Mkuu naye 
alielezwa majukumu yanayotekelezwa na Mfuko ambapo Afisa Uhusiano 
Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Sebera Fulgence, alimueleza kuwa sekta ya 
viwanda na biashara ni miongoni mwa sekta zinazotoa wanachama wengi 
kwenye Mfuko huo, ukiachilia elimu na afya na kwamba Mfuko umekuwa 
ukiendelea kutoa elimu zaidi kwa waajiri kuhusu umuhimu wa kuchangia 
wafanyakazi wao kwa manufaa ya mwajiri na mwajiriwa pindi yanapotokea 
madhara. Mfuko wa WCF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa 
mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (sura 263 
marejeo ya mwaka 2015).

 Profesa
 Ibrahim Hamisi Juma, akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa 
yakitolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera 
Fulgence.(hayupo pichani)

 Afisa
 Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia
 maeelzo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma 
(kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF. 

  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera
Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli
zifanywazo na WCF.
Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli
zifanywazo na WCF.

 Waziri
 wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizungumza 
jambo na Maafisa wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto) ambaye ni 
Afisa Uhusiano Mwandamizi na Bi.Bi.Inocencia William

 Mhe. Waziri Mwijage, (kulia), akiagana na Bw. Sebera baada ya kutembeela banda hilo na kuelimishwa kuhsuu majukumu ya Mfuko.

 Maafisa wa WCF wakiwa tayari kuwahudumia wananachi 

 Bi.Bi.Inocencia William, (kushoto), afisa wa WCF akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda la Mfuko huo

 Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za shughuli na majukumu yanayotekelezwa na WCF


Mhe. Profesa Hamisi akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka

 Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto) akiaghana na wafanyakazi wa WCF

Bw. Sebera akisalimiana naMchambuzi wa soka hapa nchini, Bw. Ally Mayai kwenye banda la Mfuko wa WCF
Post a Comment