
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akielekea
 kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya Agricom 
akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric 
Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya 
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya 
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es 
Salaam.
Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa.

Meneja
 Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa 
maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
 Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) 
alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa 
yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere 
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
 Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) 
akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – 
TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea 
huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea 
katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) 
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mratibu
 wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni wakopeshaji wa 
zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya Agricom, Erasmus 
Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos Rweikiza 
aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya 
Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K
 Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akiwa 
ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania
 (TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto) alipowasili kwenye banda la 
TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja
 wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya 
Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
 wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd, wauzaji wa vito 
vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya 
Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la 
TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
 Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara 
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Picha
 juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF 
Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye 
banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa 
yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba 
Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni 
Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC).



Mkurugenzi
 wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa za kutunza 
ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya bidhaa halisi za
 kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – 
TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41
 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya 
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es 
Salaam.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitoa 
maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati akitembelea banda
 la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho ya 41 ya Biashara
 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya Biashara wa Mwl J.K 
Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni 
Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) 
Jacqueline Maleko.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi 
akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake 
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya 
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti
 wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimuongoza 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald 
Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 
ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi 
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft, Culture
 & Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la EOTF 
kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika 
Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara 
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi 
akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda la 
EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja
 wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya 
Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa
 kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi 
akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea
 kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
 yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere 
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni 
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisaini
 kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu 
lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara
 ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere 
(Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi 
akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za 
Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa 
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

Mwenyekiti
 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata 
maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka 
kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women’s Bank, Renita Michael 
(kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya 
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya 
Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es 
Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), 
Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake 
Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
Post a Comment